KIKOSI cha Simba kimewasili salama ardhi ya Bandari Salama, Dar leo Desemba 25 kutoka nchini Zimbabwe.
Desemba 23 kilikuwa Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe kikisaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwenye mchezo huo kikosi hicho kilipoteza kwa kufungwa bao 1-0. Bao hilo la ushindi kwa FC Platinum ya nchini Zimbabwe lilipachikwa kimiani na Perfect Chikwende dakika ya 17.
Kimerejea kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya kuanza mbio za kutetea taji la Kombe la Shirikisho ambapo Jumapili, Desemba 27 kitamenyana na Majimaji ya Songea.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa na mshindi atasonga hatua inayofuata atakayepoteza safari itaishia Uwanja wa Mkapa.
Baba karudi kutoka kazini
ReplyDeleteNa adhabu ya bakora moja
DeleteMnataka nilie
ReplyDeleteUwiii
ReplyDeleteNyingi vyura mnawakilosha maneno hapo mngekuwa mabingwa kwa maneno ndio mana mkaitwa vyura aka kandambili
ReplyDeleteHuyu kocha apite hvi hafai kwenye club yetu
ReplyDeleteKila la heri Somba
ReplyDelete