PEP Guardiola, Kocha Mkuu wa Klabu ya Manchester City amesema kuwa Arsenal inabidi impe muda kocha wao Mikel Arteta kwa kuwa ni kocha mwenye uwezo mkubwa.
Guardiola alifanya kazi kwa ukaribu na Arteta ndani ya City kabla ya kuibukia ndani ya kikosi hicho Desemba 2019.
Arteta aliweza kushinda mara mbili taji la Ligi Kuu England na taji la FA akiwa ndani ya kikosi cha Manchester City ambapo alikuwa ni kocha msaidizi.
Ikiwa nafasi ya 15 Arsenal kwa msimu huu imekuwa kwenye mwendo jambo ambalo linampa presha Arteta.
Guardiola amesema:-"Arteta anahitaji muda ndani ya Arsenal kwa sasa kwa sababu ninamjua ni kocha mzuri na ana uwezo mkubwa wa kufundisha timu na ikapata matokeo licha ya sasa kuwa kwenye mwendo mbovu.
" Arsenal haitapata mwalimu mzuri na mwenye uwezo wa kuifundisha timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao kwa kuwa aliyepo sasa ameanza kutengeneza misingi ya timu hiyo hivyo kwangu ninaona ni mwalimu bora.
"Siwezi nikasema kwamba ninampa sapoti ili abaki, ila ukweli ni kwamba yeye mwenyewe anajua kila kitu na anauwezo wa kuwa bora zaidi ya hapo alipo. Anapenda kile anachokifanya namna anavyojitoa pamoja na kutimiza majukumu ndani ya timu yake kwa sasa," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment