December 15, 2020


BAADA ya kumaliza kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine Mbeya kwa kushinda bao 1-0 kesho ina kazi ya kusaka pointi nyingine mbele ya KMC.


Tayari kikosi cha Simba kinachonolewa  na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kimeshatia timu Dar es Salaam, jana Desemba 14 kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara. 


Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kuwa na mwendo mzuri ndani ya uwanja zikiwa kwenye viwanja vya Dar.

KMC imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar Uwanja wa Jamhuri, Morogoro itaingia ndani ya uwanja ikiwa na hasira za kulipa kisasi cha kupoteza.


Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na wanahitaji pointi tatu muhimu.


Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anaamini utakuwa mchezo mgumu ila anahitaji pointi tatu muhimu.

6 COMMENTS:

  1. Simba kwenye dirisha dogo msajirini kibu Denis yule dogo anajua

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ili Kibu aje achukue nafas ya nani, Boko, Kagere, Mugalu? au unataka mtoto wa watu aozee benchi kama Ilamfya? Acheni roho mbaya kihivyo jamani loh!

      Delete
  2. Replies
    1. Ni kwamba Simba wanajitoa ufahamu kwamba "kuzima saa kunachelewesha muda au kucha"!
      Kuomba review of the judgement hakuiondoi adhabu; wataeleweshwa tu uamzi ulifikiweje na sio kwamba Simba hawajui, ndio maana unawasikia mara Senzo, mara TFF, mara babaake. Wanadhan FIFA ni kama TFF kwa vile Mo alipeleka nanihino na Tshirt kwa Infantino? The buck stops there.

      Delete
    2. Punguza hasira.. FIFA imewapa room ya kufanya hicho wanacho kifanya!

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic