December 17, 2020




 NAHODHA wa Klabu ya KMC, Juma Kaseja amesema kuwa mashabiki wameona namna maamuzi yalivyokuwa hivyo hana cha kuzungumza kuhusu penalti ambayo waliipata Simba jana, Desemba 16 Uwanja wa Mkapa.


Kwenye mchezo wa jana, Kaseja akiwa langoni baada ya mabeki kuokoa hatari dakika ya 73 hakuwa na chaguo baada ya mwamuzi kuweka kati tuta kwa kile ambacho alidai kwamba kuna mchezaji wa KMC aliunawa mpira huo uliokuwa ndani ya 18.


Bao hilo la ushindi lilifungwa na Meddie Kagere dakika ya 77 baada ya Kaseja kushindwa kuokoa penalti hiyo ya Kagere ambaye amefikisha jumla ya mabao matano ndani ya Ligi Kuu Bara.


Akizungumza na Saleh Jembe, Kaseja amesema kuwa kilichotokea ni sehemu ya mchezo na wanawap pongezi wapinzani wao kwa kuwa wameshinda.


"Tunamshukuru Mungu tumemaliza salama mchezo wetu na hakuna majeruhi kuhusu maamuzi hakuna nitakachoweza kusema ila nina amini kwamba kila mmoja ameona na anajua ukweli upo wapi.


"Kupoteza imeshatokea hatuwezi kubadili matokeo hivyo kinachofuata ni maandalizi kwa ajili ya mechi zetu zijazo, kikubwa mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema.


Simba inafikisha pointi 32 ikiwa nafasi ya pili huku KMC ikibaki na pointi zake 21 ipo nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.

15 COMMENTS:

  1. Wapewe tu kombe. Hii ni aibu kwa familia ya mpira

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyani haoni kundule wasemavyo wahenga, ndo uto hao wamejisahau

      Delete
    2. Dah! Yani huu usimba na uyanga mpaka kwa marefali kwa hali hii mpira tanzania hautaendele mtu ana amua kujitoa sadaka hata afungiwe ila kikubwa ipe matokeo timu fulani marefali wetu hata miaka miamoja hawato enda puliza word cup ndotoooo!!!!!!

      Delete
  2. Acha hizo wapewe kombe kivipi na Yanga mmesahau penalt mliyopewa mlipochenza na Kmc

    ReplyDelete
  3. penalti zote ni sawa isipokuwa za Simba?
    kwa taarifa yako Simba huwa hawapewi kombe wanalitafuta na kulipata..Ni Yanga ndio walikuwa wamezoea kupewa makombe na Malinzi hata mwaka jana nafasi ya kimataifa walipewa na Simba...kwani walikuwa wameshinda FA cup? Eymael alisema Yanga ni mbumbumbu tena ni .... na ....

    ReplyDelete
    Replies
    1. Shida yenu ni matusi kila mahala

      Delete
    2. Matusi nimwalimu wenu Emmy na aliyekuwa msemaji wenu muro mpaka akafungiwa kwasababu ya matusi.
      Utopolo ndo waasisi wa matusi tz

      Delete
    3. Acha kuropoka kumbuka kuna kuongea na kuropoka xaxa ww una ropoka hadharani tena kwenye umma wa watu waelewa wasoka kama sisi hatuweze tukapewa ubingwa pasipo kupambana mwangu huo uongo kwan tulikua tunachukua ubingwa simba walikua hawa chezi mechi zao kwanini wasipewe wao je kunaubingwa tulipewa 2kiwa nyuma ya pointi za simba! Huo nao ni uxhamba mwangu

      Delete
    4. kuna ubingwa mlipewa na Malinzi mkiwa point nyuma ya Simba..Mchezaji Kagera Sugar alikuwa na kadi tatu... rufaa ya Simba ilitupiliwa Mabali na mashindano hayo kimataifa Yanga iliishia kupigwa nje ndani...Gor Mahia, APR , arw

      Delete
  4. wamesahau penalti waliyopewa dhidi ya Simba..Tausi la kaangukia nje ya kumi na nane..Kipyenga cha mwisho walithibitisga mbele hata Kaze alikubali ile penalti sio halalali..Wakapewa penalti walijua wanaenda nyumbani na ushindi dhuruma..Mnyama akachomoa dak 86..kama ilivyokuwa dhidi ya Simba vs As Vita..Na penalti ya KMC kule Mwanza..Hivi mnajua zisingekuwa hizo penalti za dhuruma Yanga isingekuwa inaongoza ligi..Yaani mnyamaze kimya Mungu anawaona..
    Inakuwa kama mlivyopata nafasi ya kimataifa mkawa mnacheka Simba eti UD Singo..wakaja jitoa wenyewe kwa kujifunga Zambia

    ReplyDelete
  5. Wewe paka Jenga hoja pale mwamuzi aliamua kutoa pass ya mwisho Mambo ya unakumbuka wote tukianza kukumbusha tutakesha ,ule uamuzi ulikuwa was kujitoa muhanga refa alijua anafanya nini ,hizo unazo refer ni Vichekesho .Tatizo lenu mna kumbukumbu za like ,tunaongelea mapya siyo eti mtu yupo kwenye ndoa 20 yrs anadai ahadi ya Uchumba ulnihaidi

    ReplyDelete
    Replies
    1. tukumbushane Eymael aliwaita mbumbumbu ...nyani na sokwe kazi kubweka bwee bwee baa
      lazima tukumbushane Timu iliyofungiwa kwa rushwa Afrika kwa kutoa rushwa ili wabebwe..Lazima tukumbushane penalti dhuruma haramu ya Yanga dhidi ya KMC na ile ya Yanga dhidi ya Simba..Tukumbushane zote zilitolewa nje ya kumi na nane..Tukumbushane jinsi Malinzi alivyokuwa anabeba mbeleko ya Yanga..Jengeni hoja kama mna tatizo na penalti iliyotokea ndani ya kumi na nane iweje hamna tatizo na penalti mbili ambazo zinafanya timu yenu iwe kileleni?Acheni umbumbumbu na kubweka bwee bwee

      Delete
  6. Ama hakika nyani haoni kundule! Utopolo bora wakae kimya maana hakuna timu inayobebwa nchi kama Utopolo

    ReplyDelete
  7. Uto kaeni kimyaaa mbona mnalialia nn tatizo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanalia kwasababu wanapumuliwa mgongoni na mnyama, washaanza kuweweseka hao utopolo

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic