UONGOZI wa Klabu ya KMC umesema kuwa kesho lazima waipige Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, saa 1:00 usiku.
KMC inashuka uwanjani ikiwa imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Inakutana na Simba ambayo imetoka Mbeya na kushinda bao 1-0 lililofungwa na nahodha, John Bocco.
Christina Mwagala, Ofisa Habari wa KMC amesema kuwa kila kitu kipo sawa na wanaamini watashinda kwenye mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.
Kikiwa chini ya Kocha Mkuu John Simkoko pamoja na Kocha Msaidizi Habibu Kondo kitapambana na mbinu a Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck na Seleman Matola ambaye ni msaidizi ndani ya Simba.
Christina amesema:-“Hatuna hofu na mchezo wa kesho kwa sababu tumejipanga vizuri, tunakikosi imara, wachezaji ni wazuri ambao wanaweza kukutana na timu yoyote na tukapata matokeo.
"Wachezaji wetu wapo tayari kwa ajili ya mechi ya kesho na ushindi tunahitaji hivyo lazima wapinzani wetu wapigwe kwani lipo ndani ya uwezo wetu kikubwa ni kuhakikisha kwamba tunapata alama tatu ambazo ni muhimu.
“Tunafahamu kwamba wametoka kupata ushindi dhidi ya Mbeya City, lakini hiyo haimaanishi kwamba wakikutana na KMC FC pia watapata matokeo, kwetu wakija wajiandae kisaikolojia kuwa watafungwa.
"Hata hivyo katika misimu miwili ya Ligi Kuu iliyopita, KMC FC iliweza kupoteza michezo yake yote ya nyumbani na ugenini huku ikipata matokeo ya ushindi kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa katika Uwanja wa Chamazi.
"Hivyo kulingana na rekodi hiyo, Kikosi hicho katika msimu huu wa 2020/2021 kimejipanga kuvunja rekodi hiyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba hakuna mchezo ambao utapotea na badala yake tutakwenda kuibuka na ushindi.
"Mashabiki wajitokeze kwa wingi ilikushuhudia Pira Spana, Pira Kodi, Pira mapato litakalochezwa mbele ya mashabiki zao," .
Mwandishi atakuwa ni Mnyakyusa tu."APIGIGWE"!!
ReplyDelete