KIUNGO mshambuliaji wa Klabu ya Yanga Juma Mahadhi amepekwa kwa mkopo ndani ya Klabu ya Ihefu FC inayonolewa na Kocha Mkuu Zuber Katwila.
Mahadhi alirejea kikosini mwanzoni mwa msimu baada ya kuwa nje kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu akiuguza majeraha ya goti
Kutokana na ushindani wa namba kwenye kikosi cha Yanga, imekuwa changamoto kwake kupata nafasi kwa Cedri Kaze.
Meneja wa mchezaji huyo Godlisetn Anderson, amethibitisha kuwa Mahadhi ataitumikia Ihefu Fc kwa miezi sita.
Kwa msimu wa 2020/21 nyota huyo hajapata nafasi ya kucheza mchezo hata mmoja ndani ya Ligi Kuu Bara.
Yanga imecheza jumla ya mechi 15 na kibindoni imekusanya jumla ya pointi 37 ikiwa nafasi ya kwanza.
Ihefu ipo nafasi ya 17 ikiwa imecheza mechi 15 imekusanya pointi 10 na imeshinda mechi mbili ndani ya ligi.
0 COMMENTS:
Post a Comment