MASHABIKI wa Yanga leo Desemba 15 watapata fursa ya kuona uwezo wa nyota wao mpya Saido Ntibanzokiza ambaye amesaini dili la miaka miwili kuitumikia timu hiyo yenye maskani yake Kariakoo.
Ntibanzokiza anaweza kuwa sehemu ya kikosi kitakachoanza leo Uwanja wa Malkia Liti ambao ulikuwa unaitwa Namfua kabla ya kubadilishwa jina.
Yanga itakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United ikiwa ni kwa ajili ya kuwapa nafasi wachezaji ambao wamekuwa hawapati nafasi kikosi cha Kwanza.
Singida United inapambana Kurejea ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya kushuka Daraja msimu uliopita wa 2019/20.
Ipo kundi B ambapo imecheza jumla ya mechi 7 ipo nafasi ya 9 na ina pointi mbili kibindoni.
0 COMMENTS:
Post a Comment