ALIYEKUWA mshambuliaji nyota wa vilabu vya AC Milan, Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil Robinho, amehukumiwa kufungwa miaka tisa jela na mahakama ya rufaa ya nchini Italia, baada ya kukutwa na kosa la ubakaji wa binti mdogo alilolifanya miaka saba iliyopoita nchini humo.
Robinho na rafiki yake Ricardo Falco wameripotiwa kumbaka binti huyo raia wa Albania aiishie nchini Italia kwenye ukumbi wa starehe wakati binti huyo akiwa anasheherekea kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka 23 mwaka 2013.
Wakili wa binti huyo, Jaccopo Gnochi, amesema ”hukumu hiyo ni mfano kwa wengine juu ya kulinda utu wa mwanake na kuonyesha ni jinsi gani mfumo wa sheria unavyofanya kazi”.
Robinho anakumbukwa na wafuatiliaji wengi wa soka ulimwenguni kwa kuwa na uwezo wake mkubwa wa kuuchezea mpira, kuwatoka walinzi kwa chenga kali na kufunga mabao ya kuvutia akiwa na vilabu vya AC Milan, Real Madrid, Man city na timu ya taifa ya Brazil miaka ya 2008-13.
bint mdogo alikua na miaka 23 ajabu ila acha apate stahiki yake.kumdhalilisha mwanamke ni miongoni mwa makosa makubwa
ReplyDeletePOINT HAPO NI KUBAKA TU, WENZETU HAWANA HURUMA KISA JINA LAKO
ReplyDeleteAcha atumikie maana sio kifo.
ReplyDelete