December 15, 2020

 


NAMUNGO FC imeweka wazi kuwa sababu ya kumtumia mchezaji Shiza Kichuya ambaye ilielezwa kuwa FIFA wamemfungia kucheza kwa muda wa miezi sita na Klabu ya Simba imepigwa faini kwa kumtumia mchezaji huyo kinyume na taratibu za usajili ni kutokana na Simba kuomba shauri hilo lipitiwe upya.


Kichuya alisajiliwa na Simba kwenye usajili wa Januari akitokea Klabu ya Pharco ya Misri ambao wanadai kwamba alikuwa na mkataba wa miaka miwili na alitumia mkataba wa mwaka mmoja jambo lililowafanya wapeleke malalamiko hayo kwa FIFA kulalamikia suala la usajili wa mchezaji huyo.

Ofisa Habari wa Namungo FC, Kindamba Namlia amesema, Kichuya ataendelea kutumiwa na klabu hiyo kwa sababu Klabu ya Simba imeomba FIFA kufanya mapitio upya ya shauri linalomhusu mchezaji huyo.


"Katika taarifa tuliyopewa kuhusu Kichuya inasema, Kichuya anaweza kufungiwa miezi sita endapo Klabu ya Simba itashindwa kulipa faini ndani ya siku 45.


"Mshtakiwa namba moja kwenye shauri lile Shiza Kichuya anaweza kufungiwa miezi 6, mshtakiwa namba mbili Simba SC inaweza kufungiwa kusajili kwa misimu mitatu (madirisha matatu makubwa ya usajili).


"Kwa sasa Simba imeomba mapitio ya hukumu iliyotolewa na FIFA, kwa maana hiyo kila kitu kinaanza upya hadi mapitio yatakapokamilika. Maana yake hata ule muda iliopewa Simba kulipa faini hauangaliwi hadi pale mapitio yatakapokamilika.


"Taarifa itakayotoka baada ya mapitio ndio itafanya kazi.Sisi tunajitahidi kwenda kiwekedi, baada ya kuipata taarifa kuhusu Kichuya mtu wetu wa sheria hakuwepo kwa hiyo tulisubiri hadi asome nyaraka za taarifa tuliyopewa kuhusu Kichuya na atupe tafsiri yake," .

4 COMMENTS:

  1. Mkishindwa mtanyanganywa point moja ya Yanga na za Jana so ,kwanini muendelee kumtumia?

    ReplyDelete
    Replies
    1. ATAENDELEA KUTUMIKA MPAKA MAAMUZI RASMI YA FIFA YATAKAPOTOKA, HIYO SIO LEO WALA KESHO NDUGU

      Delete
  2. Duh kinacho zungumzwa hapa sidhani kama ndivyo mambo yalivyo. Mimi nashauri tuachie wa husika waendelee kushughulikia badala ya kuanza kupotosha ukweli.

    ReplyDelete
  3. Namungo lazima watanyang'anywa point.. FIFA haijawahi kukuruouka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic