December 15, 2020

 


BAADA ya sare ya kwanza Uwanja wa Azam Complex jina la aliyewapa machozi wachezaji wa timu yake linatajwa kuwa mikononi mwa George Lwandamina. 

Kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana Desemba 14 ukiwa ni mchezo wa kwanza kwa Lwandamina ambaye amechukua mikoba ya Aristica Cioaba kukaa benchi dakika 90 zilikamilika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.

Dakika 90 hizo zilipokamilika wachezaji wa Azam FC wakiongozwa na shujaa aliyefunga mabao yote mawili, Idd Selaman, 'Naldo' walionekana wakilia kwa uchungu wa kuyeyusha pointi tatu dakika za lala salama.


Mtupiaji ambaye alisababisa machozi kwa Azam FC ni Stephen Sey alifunga bao lililoipa pointi moja timu yake ya Namungo ikiwa ugenini.


Habari zinaeleza kuwa kwa sasa Lwandamina ameanza kupiga hesabu za kumuunganisha ndani ya kikosi cha Azam FC ambacho kwa sasa kinapambana kurejea kwenye ubora wake baada ya mshambuliaji wao tegemeo Prince Dube kupata majeraha ya mkono.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit hivi karibuni aliweka wazi kwamba kuna mpango wa kufanya usajili kwenye dirisha dogo ambalo linatarajiwa kufunguliwa leo Desemba 15 ikiwa kutakuwa na mapendekezo ya mwalimu.


"Usajili ni kwa ajili ya timu kubwa nasi pia lazima tufanye usajili kutokana na mapendekezo ya mwalimu," amesema.

1 COMMENTS:

  1. Dili la promo alilokupa huyu jamaa halitaisha hadi kieleweke maana ulianza na Yanga na sasa hivi umehamia kwa Azam.Tunasubiri zamu ya Simba

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic