December 17, 2020


 KIKOSI cha Simba kesho kinatarajiwa kukwea pipa kuelekea Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.


Simba inaiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa baada ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2019/20 na tayari ilishapenya hatua ya awali kwa kuitoa Plateau United ya Nigeria kwa ushindi wa bao 1-0 walilolipata kwenye mchezo wa ugenini.


Kwenye mchezo wa pili uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Simba iliweza kulinda bao lake la Nigeria ambalo lilifungwa na Clatous Chama.


Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amesema kuwa wanatarajia kuondoka Ijumaa kuwafuata wapinzani wao na msafara wa wachezaji 22.


"Tutaanza safari siku ya Ijumaa kwa ajili ya kuwafuata wapinzani wetu FC Platinum. Nina amini tutakwenda kupambana na kufanya vizuri na msafara wetu utakuwa na jumla ya wachezaji 22.


"Hautakuwa mchezo mwepesi lakini tutakwenda kufanyanya vizuri, unajua kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika huku ushindani wake ni wa tofauti.


"Kuhusu wachezaji ambao tutakwenda nao nitaweka wazi hivi karibuni kwani bado hatujafanya tathimini hasa baada ya kumaliza mchezo wetu dhidi ya KMC, wakati ujao," .


Mchezo wa kwanza ugenini unatarajiwa kuchezwa Desemba 23 na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa Januari 6.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic