USHINDI wa mabao 2-1 walioupata Liverpool Uwanja wa Anfield mbele ya Tottenham Hotspur inamfanya mwamba, Mohamed Salah kufikisha jumla ya mabao 11 ndani ya Ligi Kuu England.
Jambo hilo linafanya vita ya kiatu cha ufungaji bora ndani ya ligi hiyo inayofuatiliwa na wengi kuzidi kupamba moto kwa msimu wa 2020/21.
Salah alifikisha bao lake la 11 dakika ya 26 na kumfanya awe ndani ya tatu bora ya watupiaji ndani ya Ligi Kuu England kwa msimu wa 2020/21.
Nyota mwingine ambaye alifikisha idadi hiyo ya mabao 11 ni Son Heung-min wa Spurs ambaye alifunga dakika ya 33.
Mbali na kufunga Salah pia ametengeneza jumla ya pasi mbili akiwa amecheza mechi 12 akiwa amepiga jumla ya mashuti 33.
Song Heung-Min yeye ametoa jumla ya pasi nne na amecheza jumla ya mechi 13 akiwa amepiga jumla ya mashuti 18. Mwingine mwenye mabao 11 ni Dominic Calvert Lewin wa Everton hana pasi ya bao ila amecheza mechi 13 na amepiga jumla ya mashuti 33.
0 COMMENTS:
Post a Comment