December 17, 2020


KOCHA Mkuu wa Simba,
Sven Vandenbroeck ameweka wazi kwamba akili zake zipo kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.

Simba imetinga hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwaondoa Plateau United ya Nigeria kwa ushindi wa bao 1-0 inatarajia kukutana na FC Platinum ya Zimbabwe, Desemba 23 nchini Zimbabwe.

Akizungumza na Saleh Jembe, Sven amesema kuwa amewapa majukumu wachezaji wake ya kutafuta ushindi kwenye mchezo huo ambao anaamini utakuwa mkubwa.

“Nadhani ipo wazi kwamba tuna kazi kubwa mbili, kitaifa na kimataifa, nikiwa kwenye mchezo wa ligi nina kazi ya kufikiria pia namna nitakavyoweza kupata matokeo kwenye mchezo dhidi ya FC Platinum.

“Kwa maana hiyo wakati mwingine huwa ninakuwa sina chaguo hasa kwenye aina ya wachezaji ambao ninapaswa kuwatumia kwa kuwa kila mmoja anahitaji kucheza ligi na pia kwenye mchezo wa kimataifa hapo utulivu unahitajika,” amesema.

Januari 6, mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa na mshindi wa jumla anatinga hatua ya makundi.

4 COMMENTS:

  1. Simba twende tukafanye vzr,tuwabebe wasiyojiweza kimataifa.

    ReplyDelete
  2. Simba twende tukafanye vzr,tuwabebe wasiyojiweza kimataifa.

    ReplyDelete
  3. Simba twende tukafanye vzr,tuwabebe wasiyojiweza kimataifa.

    ReplyDelete
  4. Simba twende tukafanye vzr,tuwabebe wasiyojiweza kimataifa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic