December 25, 2020


 KATIBU Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mngereza, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Desemba 25, 2020.

Taarifa za msiba huo zimethibitoshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi.


Aidha, taarifa za awali zinaeleza kuwa Mngereza amefariki akiwa jijini Dodoma, lakini chanzo cha kifo chake bado hakijawekwa wazi.


Enzi za uhai wake Mngereza alikuwa mstari wa mbele kwenye kupigania maslahi ya wasanii pamoja na maadali katika kazi za sanaa.


Pia alikuwa akiratibu semina kuhusu ukuaji wa tasnia ya sanaa pamoja na kupinga matumizi ya madawa ya kulevya kwa jamii kiujumla.


Pumzika kwa amani Mngereza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic