December 31, 2020


LEO Desemba 31,2020 yamebaki  masaa kadhaa kwa Neema ya Mungu tuweze kufika mwaka mpya wa 2021.


Ndani ya Ligi Kuu Bara kuna mechi ambazo zitachezwa ikiwa ni za mwisho kwa mwaka 2020 kabla ya kuukaribisha mwaka mpya, mambo yatakuwa namna hii:-


Polisi Tanzania yenye pointi 23 inamenyana na Azam FC yenye pointi 29 ngoma inapigwa Uwanja wa Ushirika,Moshi.


Mchezo huu ni wa mzunguko wa pili, ule wa kwanza walipokutana Azam Complex, Polisi Tanzania ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0.


Coastal Union ya Tanga yenye pointi 19 inamenyana na Namungo FC yenye pointi 17, ngoma inapigwa Mkwakwani.


Walipokutana Uwanja wa Majaliwa Coastal Union ilitunguliwa bao 1-0.


Tanzania Prisons yenye pointi 21 inamenyana na Yanga yenye pointi 43,ngoma inapigwa Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.


Uwanja wa Mkapa ngoma ilikuwa ni 1-1 baada ya dakika 90.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic