VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga kwa sasa wapo Mbeya wakiendelea kuivutia kasi Klabu ya Tanzania Prisons.
Yanga inakula Christimas ikiwa nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 17 na kibindoni ina jumla ya pointi 43.
Imecheza mechi zote 17 mfululizo kwa msimu wa 2020/21 kwenye raundi ya kwanza bila kupoteza baada ya kumalizana na Ihefu na kushinda mabao 3-0.
Ilipaswa Jumamosi, Desemba 26 imenyane na Singida United mchezo wa hatua ya tatu Kombe la Shirikisho Afrika ila kutokana na timu ya Singida Unite kushushwa madaraja mawili kwa kushindwa kufika kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza dhidi ya Alliance wanapenya hatua ya nne.
Meneja wa Klabu ya Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa kwa sasa wachezaji watarejea kuanza mazoezi rasmi Desemba 26.Leo wachezaji wote ikiwa ni pamoja na ingizo lao jipya, Saido Ntibanzokiza watakuwa huru
"Desemba 26 wachezaji wataanza kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo wetu wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.
"Wachezaji wapo huru tutakutana Jumamosi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, mchezo wetu utakuwa Uwanja wa Nelson Mandela hivyo utaratibu wa safari utawekwa wazi hivi karibuni," .
Msipoandika negative kuhusu simba hamuoni raha. Bila shaka mnatumika
ReplyDeleteSAIDA ANTIZOBAGIZA
ReplyDeleteKipi kasema tofauti bro simba ilifungwa haliitaj hekima hilo
ReplyDeleteBasi aandike Prison iliyotunguliwa na Simba uone anaiongelea positive
ReplyDelete