December 26, 2020


 
KOCHA Msaidizi wa Klabu ya Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa mzunguko wa pili mwendo wao ni uleule ambao wameishia mzunguko wa kwanza na upo uwezekano mkubwa wa kuongeza kasi.

Kikosi cha Yanga kimeweka rekodi kwa msimu wa 2020/21 kwa kucheza jumla ya mechi 17 bila kupoteza ambapo kimeshinda mechi 13 na kutoa sare nne.

Kipo nafasi ya kwanza na pointi 43 huku wapinzani wao Simba wakiwa nafasi ya pili na pointi 32 baada ya kucheza mechi 14 ndani ya ligi.

Mwambusi amesema kuwa wamepanga kuendelea na rekodi zao kwenye mzunguko wa pili ili kufikia malengo ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

“Tumemaliza mzunguko wa kwanza bila kupoteza hilo ni jambo zuri kwetu na mafanikio ambayo tumeanza nayo hivyo tunahitaji kuendelea na rekodi hiyo kwa mzunguko wa pili.

“Tulianza kwa kusuasua ambapo tulikuwa tunashinda bao mojamoja kwa muda mrefu ila tumekuja kwenye ule ubora wa kufunga kuanzia mabao mawili mpaka matatu hapo ndipo ambapo tunataka kuendelea kwenye mzunguko wa pili,” amesema.  

Imefunga jumla ya mabao 28 na mshambuliaji wao tegemeo Michael Sarpong ametupia mabao manne kibindoni. 

3 COMMENTS:

  1. Kongole kwenu ila kama kawaida yetu hatuhitaji maneno tunahitaji matendo kama ilivyo sasa hvyo bech la ufund viongozi,mashabiki na wachezeji waendelee kushikama hii n Ligi siku zote Ligi n ngumu mno

    ReplyDelete
  2. Kbsaa hatuhitaji maneno kikubwa kumshukuru Mungu aliyetupa sisi na kuwanyima wao, tuzidi kuombea amani, utulivu na nidhamu ktk mchezo na tusiidharau wala kuibeza time yoyote, kila timu tutakayokutana nayo owe km vile tunacheza na mtani wetu

    ReplyDelete
  3. Kbsaa hatuhitaji maneno kikubwa kumshukuru Mungu aliyetupa sisi na kuwanyima wao, tuzidi kuombea amani, utulivu na nidhamu ktk mchezo na tusiidharau wala kuibeza time yoyote, kila timu tutakayokutana nayo owe km vile tunacheza na mtani wetu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic