December 15, 2020


CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa hesabu zao kubwa kwa sasa ni kuendelea kushinda mechi zote ambazo zimebaki ndani ya Ligi Kuu Bara.


Yanga imeshinda jumla ya mechi 11 ndani ya Ligi Kuu Bara ikiwa na sare nne kwenye mechi 15 ambazo imecheza.


Leo itakuwa na kazi Uwanja wa Liti, kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United kwa ajili ya kujiweka sawa majira ya saa 10:00 jioni.


Kaze ametoka kushinda mchezo wake uliopita wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mwadui kwa ushindi wa mabao 5-0 jambo lililowafanya wazidi kujikita kileleni na pointi zake 37.


Kocha huyo kipenzi cha mashabiki amesema:"Bado kuna kazi kubwa ya kufanya mpaka kufikia ubingwa ulipo na inawezekana kufanya vizuri kwa sababu tuna mwendo makini.


"Kwenye kila mchezo kwetu ni fainali na tutapambana ili kupata matokeo mazuri, mashabiki watupe sapoti ili tuweze kufikia malengo yetu," .


Yanga imefunga jumla ya mabao 22 na kinara wa utupiaji wa mabao ni Michael Sarpong mwenye mabao manne.

8 COMMENTS:

  1. Kwa kocha mwenye weledi kauli kama hii ni dharau kubwa kwa soka letu, ina maana timu zingine hazina makocha wenye uwezo! Subiri kwani wapinzani washazisoma mbinu zako na utalalamika

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kauli gani wewe umeitafsiri kama dharau ndugu?

      Delete
    2. mimi nadhani hakuna kocha mwenye malengo ya kupoteza mechi zake zote, kila kocha lengo lake ni kushinda kila mechi ili mwisho wa msimu aibuke bna ubingwa......sasa bwana Majawa kauli iliyokosa uweledi ni HIPI?.....Alafu mwishimiwa akiwaita mbumbumbu mnapaniki

      Delete
    3. Hujaelewa kabisa. Dharau ni nini hapo !!!!!

      Delete
    4. Kauli ganiwewe unaiona kama ni dharau?..sioni hata kama kuna shida na maneno ya kocha wa yanga,na kaa ukijua kila kocha ana malengo na ligi hii,wapo wanaotaka kubaki ligi kuu,na wapo wanaodai kuchukua ubingwa wa ligi kama alivyo kocha wa Yanga na wengine pia,na wapo wanaotaka angalau kuwa nafasi 3 za juu,,tatizo la mashabiki wengine wamekaa kukariri tu..

      Delete
  2. Wewe Mtu kwani lazima u comment?

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. sisi n wavivu wa kusoma na kuyaelewa mambo kwa mapana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic