MSANII Mkongwe wa Muziki wa Dansi nchini Tanzania Papii Kocha na Bendi ya African Stars Band ’Twanga Pepeta’ wanatarajiwa kunogesha La Macarena Lounge Bonanza litakalofanyika Jumamosi hii Uwanja wa Bora, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi wa La Macarena Lounge Emmanuel Mwendapole alisema kuwa bonanza hilo linatarajiwa kushirikisha wasanii Timu ya Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (Taswa FC), Wasanii wa Bongo Movies na Twanga Pepeta.
Mwendapole alisema kuwa bonanza hilo linatarajiwa kuanza asubuhi kwa michezo mbalimbali ikiwemo mbio za magunia, kukimbiza kuku na soka kwa Taswa FC kucheza dhidi ya Team La Macarena na baada ya bonanza hilo jioni itakuwepo burudani kutoka kwa Papii Kocha na Twanga Pepeta.
“Maandalizi yamekamilika katika kuelekea bonanza hilo ambapo asubuhi kutakuwa na michezo mbalimbali ikiwemo soka, kukimbia na magunia, kukimbiza kuku na soka kabla ya jioni kupata burudani kutoka kwa Papii Kocha na Twanga Pepeta,”alisema Mwendapole.
Papii Kocha alizungumzia bonanza hilo kwa kusema kuwa “Siku hiyo nimepanga kutoa burudani ya kutosha baada ya kumaliza kutoka kucheza bonanza ambalo tumepangwa kuanza kucheza dhidi ya Taswa, hivyo watu wajitokeza kwa wingi kunishuhudia nikiwa uwanjani," .
0 COMMENTS:
Post a Comment