CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ujio wa nyota mpya ndani ya kikosi hicho, Fiston Abdoul Razack utamuongezea nguvu katika kusaka taji la Ligi Kuu Bara.
Kaze amesema kuwa anatambua uwezo wa nyota huyo hivyo hana mashaka na namna ambavyo atafanya kazi ndani ya kikosi chake hicho ambacho kwa sasa kinaongoza ligi.
Yanga ipo nafasi ya kwanza baada ya kucheza jumla ya mechi 18 na kibindoni ina pointi 44 huku ikiwa imefunga mabao 29 na kufungwa mabao 7.
Kaze amesema:"Ujio wa Razack una kazi moja ya kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji na kuifanya timu ifunge mabao mengi kwa kuwa hapo awali hapo ndipo palikuwa na matatizo.
"Kwa sasa nina amini mzunguko wa pili utakuwa wa tofauti na mashabiki watarajie kuona burudani na kazi nuzri kutoka kwa timu kiujumla," .
Nyota huyo ambaye ni raia wa Burundi amesaini dili la miezi sita akitokea Klabu ya ENPPI ya Misri anaungana na Mrundi mwenzake Saido Ntibanzokiza.
0 COMMENTS:
Post a Comment