January 22, 2021


 LICHA ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Zambia kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Januari 19 nchini Cameroon ukiwa ni wa kufuzu Chan bado Kocha Mkuu, Etienne Ndayiragije anaamini kwamba nafasi bado ipo kwa Stars.

Ikiwa ipo kundi D, Uwanja wa Limbe iliyeyusha mazima pointi tatu kwa kufungwa mabao mawili mchezo wa ufunguzi na imebakiwa na mechi mbili za kusaka ushindi.

Kesho Jumamosi pia inashuka uwanjani kusaka ushindi mbele ya timu ya Taifa ya Namibia na kete yake ya mwisho ni Januari 27 dhidi ya Guinea ambapo ili iweze kufuzu kutinga hatua ya robo fainali.

Kwa sasa ni wachezaji wawili ambao wanahitaji ripoti kutoka kwa dakatri ili kujua kama wanaweza kucheza ambao ni mshambuliaji John Bocco na beki wa kati Ibrahim Ame ambao ni majeruhi.

 Seleman Matola, Kocha Msaidizi wa Stars amesema kuwa vijana wapo tayari kwa mapambano na wana imani ya kupata matokeo.

"Mchezo wa kwanza tulianza vizuri ila makosa ambayo tuliyafanya yalitugharimu, tutayafanyia kazi ili mechi zetu zilizobaki tufanye vizuri, bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kikubwa sapoti," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic