KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedrick Kaze amesema kuwa wanahitaji kulitwaa Kombe la Mapinduzi ili kuongeza hali ya kujiamini kwa wachezaji wake.
Yanga imetinga hatua ya fainali kwa ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Azam FC baada ya dakika 90 kwenye nusu fainali ya kwanza kukamilika kwa timu hizo kufungana bao 1-1.
Bao la Azam FC lilifungwa na Obrey Chirwa na lile la Yanga lilipachikwa kimiani na Tuisila Kisinda.
Kesho Jumatano, Januari 13 zitakutana na Simba kwenye mchezo wa fainali utakaochezwa Uwanja wa Amaan, Visiwani Zanzibar.
Kaze amesema:"Malengo ni kuona kwamba tunatwaa taji la kombe hili ambalo tunashiriki kwa sasa. tunaamini kwamba haitakuwa kazi nyepesi ila tupo tayari kwa ushindani.
"Kikubwa ambacho kipo mashabiki wazidi kutupa sapoti na wachezaji ninajua kwamba watatimiza majukumu yao," .
Hii inakuwa ni fainali ya pili kwa Yanga kukutana na Simba ambapo ile ya kwanza walikutana msimu wa 2011 na Simba ilishinda mabao 2-1.
Simba nao wanalitaka kombe la Mapinduzi
ReplyDeleteHata wewe unalitaka pia au ulitaka akwambie kwamba kombe halitaki
ReplyDeleteYule sio haji manara akaongea porojo hiyo sio kazi yake yeye anakionfelea kikosi chake cha wengine watajua mwenyewe kama wataenda na paka au na bundi kazi kwao upo mtani ruksa kwenda hata na popo
ReplyDeleteKWA HIYO KILA MANAA ANAPOONGEA NI POROJO, UNA UHAKIKA KILA ANACHOSEMA KAZE YUPO SAHIHI? UMEONA ALICHOONGEA BAADA YA MECHI YA KWANZA?
DeleteLengo la kila coach ni kupata kikombe, mlitaka aseme anataka Paka?
ReplyDeleteumeanza vizuri, umemalizia vibaya
DeleteYanga wanachekesha, mtu wao aingize paka huku akijifanya simba ili waichafue simba lakini kila kitu kimebuma. Kwani kuvaa jezi za simba ni uthibitisho kuwa mtu wa simba?
ReplyDeleteIla Kaze ni mwelewa, sio yile Zahera sijui zuhura wao alikuwa anakesha kuongelea mambo ya simba anasahau hata kama yeye ni kocha wa yanga. Na ndio aliyewafundisha mashabiki uchwara wa yanga kulalamika kila kitu kinachohusu simba
ReplyDeleteAKALIIBE
ReplyDelete