IMEELEZWA kuwa kwa sasa kuna majina matatu ambayo yanatajwa kuingia kwenye orodha ya wale ambao wanatafutwa kurithi mikoba ya Sven Vandenbroeck, raia wa Ubelgiji.
Kocha wa zamani wa Al Ahly, Rene Weiler aliyepata mafanikio ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Misri, Kombe la FA la Misri kabla ya kutimuliwa hivi karibuni kumpisha Pitso Mosimane kutoka Afrika Kusini anatajwa kuwa kwenye rada za Simba.
Pia Florent Ibenge anayeinoa timu ya taifa ya DR Congo na AS Vita yupo kwenye rada za Simba.
Ibenge kwa sasa yupo Bongo akiwa na timu ya Taifa ya Congo ambayo leo inacheza mchezo wa kirafiki na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
Pia Kocha Msaidizi wa Raja Casablanca, Hicham Aboucherouane naye anatajwa kuwa miongoni mwa makocha ambao wameomba kazi ndani ya kikosi hicho ambacho kesho kitacheza mchezo wa fainali wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga.
Kwa mujibu wa Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa mchakato upo sawa na wana amini kwamba watampata mtu sahihi ndani ya kikosi hicho.
Barbara alizungumza kuwa simba haina haraka kumpata mrithi wa Seven? Sawa ila huo utakuwa ni uvivu na uoga wa kimaamuzi ndani ya uongozi wa simba kwani simba haipo katika wakati wa kawaida bali ipo kwenye nyakati za zarura sio nyakati za kurelax ni nyakati za kureact soon not later na hapa ndipo umahiri katika uongozi unapoonekana. Tunajua kocha mzuri ni gharama ila kama klabu nadhani itakuwa tayari ilikuwa na orodha ya makocha ambao kama ingetokea dharura kwa Sven basi wangekuwa wa kwanza kuwa interview.Makocha wa kiarabu wazuri ila wanausumbufu kwa klabu zetu hizi za kwetu.Ibenge ni kocha wa vita na ni mpenzi pia wa klabu hiyo ambayo wapo kundi moja na simba sidhani kama inaingia akilini kwa sasa simba kumuajiri huyu kocha.Simba wanae matola amabae naamini ndie long time coach solution kwa simba hivyo ni busara kutafuta kocha mwenye uzoefu hata kama atakuwa wa gharama kwa kipindi hiki maalum yaani short time solution akiwa na kazi mbili kuisaidia simba kufanya vizuri caf champion league na kumpatia suleimani Matola muda wa kujifunza zaidi kimataifa. Sina wasiwasi hata kidogo na uwezo wa matola kwenye ligi kuu. Simba wanatakiwa kumuandaa matola kivitendo kwenye kozi za ukocha ili kukizi vigezo vya kimataifa. Kuhusu wachezaji wa ziada wa kuwasaidia simba kipindi hiki kimataifa viongozi wa simba wanatakiwa kumfuatilia kiungo Mkomoro Yousef Mchangama kama anapatikana. Mchangama miaka 30 ila kimataifa anabalaa na ataisaidia sana simba klabu bingwa Africa.
ReplyDeleteKocha msaidizi wa Raja Casablanca atawezaje kuwa kocha mkuu wa Simba
ReplyDeleteHuyo hata faa Walete kocha anaeeleweka vizur pamoja na mafanikio yake.
ReplyDeletePoint hiyo ya kwanza
ReplyDeletePoint hiyo ya kwanza
ReplyDeletePoint hiyo ya kwanza
ReplyDeleteNitawashangaa sana viongozi wa Simba kutuletea makocha wa majaribio kina Hicham Aboucheroune.Viongozi wanapaswa timu zote ndani ya makundi sio Ihefu hivyo wasije wakafanya vihoja vya kuleta makocha wa kujifunzia Simba kama Sven.Ni kheri kuvunja bank na kuleta makocha wa Kariba ya kina Lenchantre,Rene Weiler, Milovan Circovic,Kupornovic na ikishindikana mrudisheni Aussems.
ReplyDeleteIBENGE HAWEZI KUCHUKULIWA, RENE WEILER ANAPEWA NAFASI YA KWANZA, NI MOJA KATI YA MAKOCHA AMBAO HABARI ZAO ZILIANDIKWA NA GOAL.COM KUHITAJIKA NA SIMBA. MATOLA MZURI LAKINI BADO SANA, ANATAKIWA KUJIFUNZA SANA
DeleteAusems hafai mzee wa mbinu moja peke yake.Simba inafungwa hamsa 5 hamsa 5 Mara tatu ugenini hajui Nini Cha kufanya yaani 4 za mazembe ugenini ni tano pia.Sven tulimchukulia poa Tanzania ila ni bonge la kocha na analifahamu soka la Africa. Ausems hawezi kuvaa hata soksi za Sven.
ReplyDelete