BAADA ya kutoka suluhu dhidi ya Jamhuri FC, Kocha Mkuu wa Yanga, Mrundi Cedric Kaze amepanga kukifanyia maboresho kikosi chake katika mchezo ujao wa Kombe la Mapinduzi akiahidi kushusha ‘full’ mziki akiwemo Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’.
Yanga katika mchezo uliopita wa Kundi A, uliopigwa Jumanne kwenye Uwanja Amaan, Zanzibar ililazimishwa suluhu na Jamhuri huku kila timu ikishindwa kutumia nafasi ambazo imezipata.
Katika mchezo huo, kocha huyo aliwatumia wachezaji baadhi ambao walikuwa hawapati nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo baadhi yao ni Waziri Junior, Adeyum Saleh, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Said Makapu na Farouk Shikalo.
Kaze ameweka wazi kuwa walishindwa kupata matokeo kutokana na uimara wa wapinzani wao ikiwa ni pamoja na kipa Nasoro Twaliba ambaye alijitahidi kuokoa michomo golini kwake.
Kaze alisema kuwa katika kuelekea mchezo ujao dhidi ya Namungo FC utakaopigwa leo Ijumaa hii saa 2:15 kwenye Uwanja wa Amaan, amepanga kukifanyia maboresho kikosi chake kwa kuwaanzisha wachezaji wake tegemeo ili wapate matokeo mazuri ya ushindi.
Aliongeza kuwa kikubwa amepanga kulichukua kombe hilo ambalo anaamini kwake litamjengea heshima kubwa na kuwapa furaha mashabiki wa timu hiyo ambao wamekuwa wakiwasapoti katika michezo mbalimbali.
“Tumekutana na timu nzuri ya Jamhuri inayocheza soka safi la kuvutia, kiukweli sikutarajia kukutana na upinzani mkubwa ambao kwangu ni somo tosha.
“Hivyo, tunajipanga kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya Mapinduzi, siyo mchezo mwepesi, kwani tunajuana vizuri na Namungo siyo mechi nyepesi.
"Hivyo ni lazima kikosi changu kiwe na mabadiliko kidogo kwa kuwaanzisha wachezaji wangu wote tegemeo akiwemo Saido ambaye yeye hakucheza kabisa mchezo uliopita dhidi ya Jamhuri,” amesema Kaze.
Naye, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela alisema: “Sisi tunalitaka ili kombe msimu huu kama nyama, wala hatuna mzaha kabisa, kutoka sare kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Jamhuri kusiwafanye watu wakaamini kuwa hatupo ‘serious’, jamani tupo makini kweli.
Leo Saida lazima acheze, hatutaki kuharibu brand yetu
ReplyDelete