January 1, 2021


 KIUNGO mshambuliaji wa Simba raia wa Msumbiji, Luis Miquissone, ndiye anayeongoza kukunja mshahara mkubwa kwa wachezaji wanaocheza Ligi Kuu Bara msimu huu.

 

Inaelezwa kuwa, kiungo huyo anayetumia zaidi mguu wa kushoto, anachota dola 7,000 (zaidi ya Sh 16 Mil) kwa mwezi.


Staa huyo ndani ya Simba pia ndiye anayeongoza kwa wachezaji wa timu hiyo wanaovuta mkwanja mrefu.

 

Luis alijiunga na Simba katika usajili wa dirisha dogo msimu uliopita, alikuwa akiitumikia kwa mkopo UD Songo inayoshiriki Ligi Kuu ya Msumbiji.Kiungo huyo kabla ya mechi ya amefunga bao moja huku akipiga asisti saba ndani ya Ligi Kuu Bara.


Cheki ‘Top Five’ ya wachezaji wanaolipwa mishahara mikubwa ndani ya Ligi Kuu Bara msimu huu kati ya hao wanatoka klabu za Simba na Yanga, Luis ndiye anayeongoza kwa kuvuta mkwanja mrefu.

 

Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ ndiye anayefuatia kwa kuchukua mshahara mkubwa ambaye kwa mwezi anaweka kibindoni Sh 13 Mil.

 

Saido ataanza kuchukua mshahara huo mwishoni mwa mwezi huu baada ya kujiunga na timu hiyo wiki mbili zilizopita ambaye alisajili katika dirisha dogo lililofunguliwa hivi karibuni.

 

Kiungo mchezeshaji wa Simba raia wa Zambia, Clatous Chota Chama, anafuatia akichota kitita cha Sh 13 Mil sawa na Saido, hivyo upo uwezekano mkubwa wa dau hilo kuongezeka katika msimu ujao kama ataendelea kubakia hapo au kuondoka na kujiunga na Yanga.


Mukoko Tonombe wa Yanga, naye ameingia katika orodha hiyo ambaye anachukua mshahara wa Sh 12Mil sawa na Mkongomani mwenzake Tuisila Kisinda waliojiunga pamoja na Yanga wakitokea AS Vita ya DR Congo.

 

Nyota hao ni kati ya wachezaji wanaounda kikosi bora cha Yanga ambacho kimeipa matokeo mazuri ya ushindi na kuifanya timu hiyo kukaa kileleni katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 44 ikicheza michezo 18.

 

Mnyarwanda wa Simba, Meddie Kagere yeye analipwa Sh 11 Mil kila mwezi, alifanikiwa kuchukua ufungaji bora katika misimu miwili mfululizo akiwa na timu hiyo.Mshambuliaji huyo amekuwa tegemeo katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo sambamba na John Bocco na Chris Mugalu.


Chanzo: Spoti Xtra

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic