January 1, 2021


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa upo kwenye mpango wa kukamilisha usajili wa mshambuliaji mmoja ambaye atakuja kuongeza nguvu ndani ya kikosi hicho akisaidiana na nyota wengine waliopo ndani ya kikosi hicho.


Yanga inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa imecheza mechi 18 bila kupoteza kwa msimu wa 2020/21 ikiwa imekusanya pointi 44.

Mchezo wake wa mwisho ndani ya 2020 ilimaliza kwa kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Tanzania Prisons, mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.

Mkurugenzi wa Uwekezaji ndani ya Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga, Injinia Hersi Said amesema kuwa mipango ipo wazi na watamtambulisha nyota huyo hivi karibuni.

"Kila kitu kuhusu usajili wa mchezaji wetu mpya upo tayari na atakuja kuongeza nguvu kikosini, kikubwa mashabiki wasiwe na mashaka tutafanya vizuri.

"Hatuwezi kumuweka wazi kwa sasa kwa sababu ni makosa ambayo tumewahi kuyafanya siku za nyuma wachezaji wetu wakapata matatizo, kilichopo kwa sasa ni kuona kwamba wachezaji wanakuja baada ya kukamilisha utaratibu," amesema.


Jembe ambalo linatajwa kuwa kwenye hesabu za Yanga ni Ferebory Dore raia wa Congo ambaye amecheza soka la kulipwa kwa mafanikio nchini Ufaransa.

7 COMMENTS:

  1. Wachezaji watafika 60

    ReplyDelete
  2. Hata wafike 100 Kwan hela unalipa wewe? Nguruwe fc we tulia

    ReplyDelete
  3. Kusajili uto wanasajili.na.point wanaendelea kudondosha mojamoja.

    ReplyDelete
  4. Matatizo yapi waliyowahi kukumbananayo na wachezaji gani hao?

    ReplyDelete
  5. Mimi nawasifu jamaa hawa kuwa wameyasomea matusi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic