KAIMU
kocha mkuu wa Klabu ya Simba, Seleman Matola amethibitisha kuwa kiungo
mshambuliaji Bernard Morrison yupo fiti baada ya kupona majeraha
yaliyokuwa yakimsumbua.
Morrison hajaonekana akiichezea
Simba tangu Desemba 5, mwaka jana alipocheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United ya Nigeria huku sababu mbalimbali ikiwemo
majeraha zikitajwa.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa New Jos, Simba ilishinda bao 1-0 ambalo lilifungwa na Clatous Chama, mwamba wa Lusaka.
Akizungumza kuhusiana na afya
ya Morrison, Matola amesema: "Bernard Morrison alikuwa akisumbuliwa na
majeraha kwa muda mrefu, lakini kwa sasa hali yake imeimarika na atarejea
uwanjani kuanzia kesho Jumatano," .
Kesho Jumatano, Simba itacheza
fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Yanga katika Uwanja wa Amaan visiwani Unguja.
Ikiwa imecheza mechi tatu ndani ya Kombe la Mapinduzi na kufunga mabao saba, Morrison hakuanza kwenye mchezo hata mmoja Uwanja wa Amaan.
Pia kwenye mchezo wa kimataifa wa mwisho kukaa benchi kwa Sven Vandenbroeck ambaye amebwaga manyanga alikuwa amekaa kwa mashabiki wa VIP B akishuhudia namna wachezaji wake wakishinda mabao 4-0 dhidi ya FC Platinum.
Rudi uwanjani mzee wa kuwakera, hadi watapike
ReplyDeleteHuyo urojo atamkera nani nyie mikia aka paka mweusi
DeleteKwani hizi ni mechi za masela?Nani asiyejua kwamba huyu ni mchezaji was Simba? Ana jipya gani?Hiyo midomo yenu ujuaji mwingi angalia Drc wanavyotuenyesha mje muanze kusifia Hiyo mitumba yenu.
ReplyDeleteKwani DRC wanacheza na simba? Kaseke, fey toto, yasin ni wachezaji wa simba? Acheni hizo
ReplyDeleteTapika kama tayari umekereka
ReplyDeleteBahati mbaya tunatofautiana uelewa ,unadhani anakerwa Nani shida hapa ni utandalelism mmekulia kwenye maji machafu ,ungeangalia ITV ukaona msisiri B madimbwi ya kijani nadhani ukikulia huko utakuwa na mawazo ya eti kuwakera always
ReplyDeleteAcha dharau wewe. Kwanza kitendo tu cha kusema ungeangalia ITV, nishakuona mshamba kweli. Kwa hiyo wewe bila itv huwezi jua dunia inavoenda? Acha mawazo mgando
DeletePaka fc bhana wameshaanza kuingiwa na hofu ya mechi,Mara Morrison alikuwa na malaria mara majeraha, acheni kuangaika leo Kisinda lazima auwe mapaka ya simba tu.
ReplyDelete