January 22, 2021


 STEVE Keane mwenye miaka 53 aliletwa duniani Septemba 30 1967 sehemu ambayo alizaliwa ni Glasgow,Scotland.

Inaelezwa kuwa ni miongoni mwa waliotuma CV zao kati ya wale makocha 50 ambao waliomba kazi ya kukinoa kikosi hicho kinachoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Anapewa chapuo kubwa la kurithi mikoba ya Sven kwa kuwa ana uzoefu mkubwa na CV yake imeonekana kuwakosha mabosi wa Simba.


Nafasi yake ambayo alikuwa anacheza zama zake za mpira ni winga ambapo timu ya Naval msimu wa 1991 rekodi zinaonyesha kuwa alicheza jumla ya mechi 35 ila hakufunga bao hata moja.

Msimu wa 1988-1991 alicheza ndani ya Klabu ya Academica Coimbra ambapo alicheza jumla ya mechi 9 na alitupia bao moja.

Miongoni mwa timu ambazo amezifundisha ni pamoja na Blackburn Rovers msimu wa 2010-2012,2013-17 alikuwa ndani ya DPMM FC.

Anatajwa kuibukia ndani ya Simba kurithi mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye alibwaga manyanga Januari 7 na kwa sasa yupo zake ndani ya FAR Rabat ya Morroco.

Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe kuhusu suala hilo amesema kuwa wapo kwenye mchakato mipango ikiwa sawa kila kitu kitawekwa wazi.

3 COMMENTS:

  1. Nashauri Mwandishi usiandike kwanza habari za Simba hasa Makocha maana unatubabaisha sana.

    ReplyDelete
  2. Waandishi vwaache kueneza uongo kwa wasomaji wao

    ReplyDelete
  3. Ikiwa sisi wenyewe Simba tunaweka mambo yetu siri na bila ya majisifu, sio kama wale wengineo, ni vipi tena wengineo wamekuwa wakijaribu kuzipata siri na kuzieneza na mara nyingi kuandikia ya uongo. Sisi Simba hatujisifu kwasababu ni aibu. Kizuri kinajiuza wenyewe bila ya kujitia mnadani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic