JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa anayepaswa kulaumiwa kwa timu yake kufungwa bao 1-0 dhidi ya Burney ni yeye mwenyewe kwakuwa anapaswa kuwajibika kwa hilo.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England kwa sasa wanapitia kipindi kigumu ndani ya Ligi Kuu England kwa kuwa hawajaonja ladha ya ushindi kwa muda mrefu na mchezo wao uliopita dhidi ya Manchester United waligawana pointi mojamoja na Manchester United kwa sare ya bila kufungana.
Ilimaliza mchezo ikiwa na umiliki wa mpira asilimia 72 na ilipiga jumla ya mashuti 27 yaliyolenga lango yalikuwa 6 huku wapinzani wao wakipiga jumla ya mashuti 6 na manne yalilenga lango ila haikuwa bahati ya kupata ushindi kwa kuwa ilifungwa bao moja usiku kwa penalti iliyofungwa na Ashley Barnes dakika ya 83.
Burney wamevunja rekodi ya Liverpool ya kucheza jumla ya mechi 68 bila kufungwa ambapo mara ya mwisho kufungwa ilikuwa ni Aprili,2017 kufungwa ikiwa nyumbani jambo ambalo limemfanya Klopp asiwe na chaguo zaidi ya kukubali matokeo.
Kichapo hicho kinaifanya Liverpool ibaki na pointi zake 34 ikiwa nafasi ya nne huku Burney ikiwa nafasi ya 16 na pointi 19 na kinara ni Manchester United ambaye amekusanya jumla ya pointi 40.
Klopp amesema :"Tumepoteza mchezo nadhani ilikuwa ni jambo gumu ambalo lilikuwa haliwezekani ila imetokea ninapaswa kulaumiwa mimi kwa kuwa vijana walipambana kutimiza majukumu yao ila bahati haikuwa kwao.
"Tulikuwa na mpira asilimia kubwa na tulitengeneza nafasi nyingi ila hatukuzitumia kwa hali hii ni sawa maamuzi ambayo ninaweza kufanya yanaweza kuwa magumu lakini hakuna chaguo kwa kuwa hali imeshatokea na haiwezekani kubadilika,".
"Nilisema kwenye mchezo wetu uliopita kuna jambo ambalo halifanyi kazi ila ni lazima tufanye kazi kwa uharaka na kurejea kwenye ubora wetu," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment