January 31, 2021


MTENDAJI Mkuu wa Simba, (CEO) Barbara Gonzalez amesema kuwa mashabiki wanastahili pongezi kwa kujitokeza kwa wingi kuwashuhudia mabingwa wapya wa Simba Super Cup, Simba kwenye mchezo wa kilele cha mashindano hayo ambayo umemalizika leo Januari 31, Uwanja wa Mkapa.

Mashindano hayo ambayo yameshirikisha timu tatu ambazo ni Simba wenyeji, Al Hilal na TP Mazembe yalianza Januari 27 ambapo Simba walianza kwenye mchezo wa ufunguzi kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal.

Al Hilal ilishinda mabao 2-1 dhidi ya TP Mazembe Januari 29 Uwanja wa Mkapa na kujikusanyia jumla ya pointi tatu huku Mazembe wakiwa na pointi moja wakiwa nafasi ya tatu.

Al Hilal ambao ni mabingwa wa pili pamoja na TP Mazembe wamepewa zawadi zao pamoja na medali Uwanja wa Mkapa.

Pia kulikuwa na zawadi ya mchezaji bora ambayo imekwenda kwa Rarry Bwalya huku mfungaji bora akiwa ni Bernard Morrison mwenye mabao mawili.

Luis Miquissone alikuwa mchezaji bora wa mchezo wa leo na kipa bora ametoka ndani ya Klabu ya Simba ambaye ni Beno Kakolanya akiwa amecheza mechi mbili na kufungwa bao moja.

13 COMMENTS:

  1. tumshukuru mungu jambo limeisha salama
    wanaoteseka wako wapi?

    ReplyDelete
  2. Kwa lipi? Maigizo? Hehehe

    ReplyDelete
  3. Mambo mazuri sana na waigaji waige kila analofanya Mnyama

    ReplyDelete
  4. Sijawahi kuona steering wa picha akafa, yaan Kombe mliandae nyie, halafu mshindwe kulichukua? Basi ungekuwa ukichaa...happy kulikuwa hakuna mashindano ya kombe, Bali danganya toto, subirin mziki wa As vita Feb 13, ndo mtajua Kat ya mbivu na mbichi ni zipi

    ReplyDelete
    Replies
    1. ...yes akipigwa risasi anainuka.. jiji limepoaa

      Delete
    2. Vita wakifungwa utasikia Aah AS VITA Hawa sio wale,kwa Simba hii Kuna mtu atazimia anayetegemea Simba itafungwa na Vita watakuwa wanalala mapema sana

      Delete
  5. Utopolo mtashangilia timu za nje miaka 10 back to back. Mpaka mmalize jezi za timu za nje zote.Utopolo uhasidi ni jadi yenu.

    ReplyDelete
  6. Roho kama inakuuma Utopolo nunua kamba jitundike.Pathetic.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe ndio faraa kweli, kama imekuuma sisi kusema bonanza jitundike wewe basi

      Delete
    2. Utopolo vinywa vyenu vimejaa matusi ndo maana hamuendelei

      Delete
  7. Ni kama kweli utopolo roho inamuuma kila Mnyama anapotia nuru basi ajipige kichwa chake na ukuta

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic