KOCHA mkuu wa klabu ya Simba, Didier Gomes Da Rosa amesema kuwa mchezo uliopita dhidi ya Azam umewasaidia kujua mapungufu waliyonayo na kuyafanyia kazi kabla ya kuivaa AS Vita.
Juzi Jumapili Simba ililazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya
Azam katika mchezo mkali wa kiporo cha Ligi Kuu Bara uliopigwa katika dimba la
Mkapa jijini Dar es Salaam.
Simba imeondoka nchini leo kuelekea DR Congo kwa ajili ya
mchezo wao wa kwanza wa kundi A, hatua ya makundi, Ligi ya mabingwa Afrika
utakaopigwa siku ya Ijumaa.
Akizungumza muda mfupi kabla ya kuondoka nchini Gomes
amesema: “Kwenye mchezo dhidi ya Azam tuliacha eneo kubwa wazi na kuwafanya wapinzani
wetu watushambulie zaidi.
“Lakini pia tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga ambazo
tulishindwa kuzitumia, hivyo kuelekea mchezo huu dhidi ya AS Vita tumerekebisha
makosa hayo na nina imani kubwa makosa hayo hatutayarudia,"
Sio wametukumbusha, sema wametuonyesha. Wamewakumbusha kwani waliyasahau? Tumie kiswahili fasaha
ReplyDeleteKwan we ndo kocha... Kocha ndo anajua Kama wamesahau ama la. Umetoka ku puu hko unavamia tu unataka kujifanya we ndo unajua Sana.
DeleteHaya wewe unayejua hongera
ReplyDeletetatizo kocha hakufanya maamuz sahihi kweny sub. mwenzak kaimarisha kiungo yy akaua kiungo kuimrisha foward
ReplyDeleteKocha anajua afanye nini mechi na Azam huku akijua pia anapaswa kuwa na tahadhali gani mechi inayofuata na Vita Club. Sisi wapenzi tunajua la Azam tu. Tumuache yeye ndio mwisho wa siku anawajibika.
ReplyDelete