KOCHA mkuu wa klabu ya Yanga,
Cedric Kaze ameamua kumbadilishia majukumu kiungo mshambuliaji wa klabu hiyo
raia wa Angola, Carlos Carlinhos kwa kumtoa katikati na kumtaka acheze kwa
kutokea pembeni.
Licha ya kutumika kama namba kumi kwa muda mrefu tangu atue ndani ya kikosi cha Yanga, lakini katika mchezo uliopita wa kujipima nguvu dhidi ya African Sports uliopigwa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi, jijini Dar es Salaam Carlinhos alionekana akicheza kutokea pembeni.
Kuhusiana na maamuzi hayo kocha Kaze
amesema kupitia mbinu zake anadhani Carlinhos atakuwa bora zaidi akicheza
katika eneo la pembeni, kulinganisha na katikati.
“Carlinhos katika mbinu zangu
amekuwa akionyesha kiwango kizuri zaidi anapocheza akitokea pembeni
kulinganisha na anapotokea eneo la katikati ya uwanja, na baada ya kurejea nimepanga kumtumia zaidi katika eneo hilo kwa kuwa nadhani atafanya makubwa,”
0 COMMENTS:
Post a Comment