February 25, 2021


 BAADA ya uongozi wa Yanga kumpa Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara muda wa siku 14 za kuomba msamaha na ikiwa atashindwa watampeleka mahakamani, Manara amesema kuwa hawezi kufanya hivyo kamwe.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredric Mwakalebela hivi karibuni aliweka wazi kuwa wanampa siku 14, Haji Manara za kuomba msamaha hadharani kwa kuwa alitumia vibaya mtandao wake wa kijamii kuishusha hadhi jezi ya Yanga.

Mwakalebela alienda mbali kwa kusema kuwa kwa kufanya hivyo kulipunguza mauzo ya jezi za Yanga jambo ambalo wanalihitaji kutoka kwa Manara ni kuomba msamaha hadharani.

"Tunampa Manara (Haji) siku 14 za kuomba msamaha kwa ajili ya kutumia jezi ya Yanga kinyume na utaratibu katika mtandao wake wa kijamii kwa kuweka chapisho ambalo limefanya mauzo ya jezi kushuka.

"Ikiwa hatafanya hivyo siku hizo zikikamilika basi tutachukua hatua ya kwenda mahakamani kumfungulia mashtaka,".

Manara amesema:"Mimi kuomba msamaha siwezi kabisa, haiwezekani jambo hilo kutokea kwa sasa kwani nimezoea kesi tena kesi kama hizi acha kabisa,".

Yanga walitoa kauli hiyo Februari 19,hivyo itakapofika Machi 5 zitakuwa zimekamilika siku hizo 14 ambazo Manara amepewa na mabosi wa Jangwani.

12 COMMENTS:

  1. Kwani ile jezi ya Mirrison imeshamalizika? Ni bora kushughulikia timu ambayo inasuwasuwa kuliko kushughulikia Manara kwa jambo ambalo linatokana na utani wa jadi

    ReplyDelete
  2. Mwakelebela hana jipya, anajitahidi kuwadanganya mashabibi wa Uto.Watanshtukia muda si mrefu,watamtoa na Bakora pale Jangwani.

    ReplyDelete
  3. Na hizo kilo 700 sijui atakimbiaje hizo bakora.

    ReplyDelete
  4. unaweza sema namna Simba walivyomchukua Morrison ni utani kati ya Simba na Yanga...
    Aende mahakamni hatopata chochote kwani kilichotokea ni utani

    ReplyDelete
  5. Inawezekana Manara yupo sawa kwa akili ya Watu wa Aina yake .Lakini kwa level yake na nafasi aliyo nayo kwa Club ya Simba Mambo mengine asingefanya .Hapa kwetu utani unazidi na hatujui madaraka na Uongozi ni nini.Nawambia ukweli haitatokea Simba hata Kama Wacheze club Bingwa Final useme kima Cha chini Kiingilio ni Tzs 50,000/ikapata Watu wa kujaza uwanja cse Manara amejenga taswira ya kujaza Uwanjani kwa 5,000/na vigoma kisa kuwakomoa Yanga japo kuwa naamini wapo Simba wasiopenda Ushambenga au vigoma wanaweza kujaza Uwanjani kwa Tzs 50,000/.Kwahiyo hayo malalamiko ya Yanga kwa watu wa Simba wa hicho kima Cha 50,000/plus wanaelewa maana ya biashara na wengi hawaendi viwanjani Lakini wanafatilia mpira,Hawa wanywa Mo energy and viroba wao kwao hawaoni hathari ya tamko Lile ndiyo maana wanafurahi,na ndiyo wanaojaa viwanjani.

    ReplyDelete
  6. Ni kweli Manara umezoea kesi tukianzia na zile kesi za utapeli wakati enzi zile ulipojishikiza CCM ili upate mkate wako wa kila siku,then kuna ile kesi ya kuwatapeli wenye magari ya kukodi nayo sijui iliishia wapi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Chuki binafsi haifai eeh tuiacheni jamani italeta tafarani Twanga pepeta hao

      Delete
    2. Sio chuki binafsi bali ni yeye mwenyewe ndo ametamka kulingana na uzoefu

      Delete
  7. jamani tafadhalini jama mbona inaonekana kama vile huu utani wa Simba na Yanga unaelekea pabaya umekuwa sio utani tena bali ni uhasama na vita ambavyo vina uadui ndani yake, tafadhalini tena chonde chonde watanzania wenzangu mpira ni burudani na vita guys,

    ReplyDelete
  8. Nyani(utopolo) haoni kundule mkamuulize Jerry muro kipindi akiwa msemaji wa utopolo alifanya nini na Sasa utopolo mnasema nini ufahamu wenu bado niwakitoto mkikua mtaacha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic