February 19, 2021

 


FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Klabu ya Biashara United amesema kuwa licha ya kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba,  jana Uwanja wa Karume ameridhishwa na viwango vya wachezaji wake. 


Ikiwa Uwanja wa Karume,Mara ilikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 lilipachikwa dakika ya 21 na kiungo wa Simba, Bernard Morrison kwa pasi ya Said Ndemla. 


Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 42 ikidaiwa pointi nne na Yanga iliyo kileleni na pointi zao ni 46 baada ya kucheza mechi 20 huku Simba ikiwa imecheza mechi 18.

Biashara United ya Mara ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa imecheza jumla ya mechi 20 na ina pointi 32.

Baraza amesema:"Tumepoteza mbele ya Simba hilo lipo wazi ila wachezaji wangu wamecheza vizuri na wameonyesha kwamba wapo fiti asilimia 100.

"Ndani ya uwanja walikuwa hawajidondoshi wamecheza kwa utulivu na kwa nidhamu hivyo kwa sasa tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu zijazo,".

Wamekutana na Simba mara mbili msimu wa 2020/21 na zote wameacha pointi tatu  na kufanya jumla wapoteze pointi sita na kufungwa mabao 5-0, Uwanja wa Mkapa ilikuwa 4-0 na Uwanja wa Karume 1-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic