February 1, 2021


 EDEM Mortotsi kocha wa viungo wa Klabu ya Yanga amesema kuwa anaamini kuwa timu hiyo italeta ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho pamoja na mashindano mengine ambayo watashiriki.

Kocha huyo anaungana na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ambaye ni raia wa Burundi kuwanoa vinara wa Ligi Kuu Bara, wakiwa na pointi 44 baada ya kucheza mechi 18.

 Tayari kikosi hicho kimeanza mazoezi Januari 25 kwa ajili ya maandalizi ya mechi zao ikiwa na ingizo jipya la wachezaji watatu kwenye dirisha dogo ambao ni Fiston Abdulazack, Saido Ntibanzokiza na Dickson Job.

Mortotsi amesema:"Nimeona kwamba wachezaji wana morali na kila mmoja anapenda kufanya vizuri ndani ya uwanja hivyo ni mwanzo mzuri kwetu na wachezaji pia.

"Imani yangu ni kwamba tutakuwa na mwendo mzuri na tutaweza kufikia malengo ambayo tumejiwekea hivyo mashabiki wazidi kutupa sapoti," .



4 COMMENTS:

  1. Why kombe la shirikisho? Can you please clarify?

    ReplyDelete
    Replies
    1. maelezo ntayapata kwa mwandishi we endelea na kazi zako, kama unazo!

      Delete
  2. Kwanza mlisema tutabeba makombe yote, sasa tutafanya vizuri. Sasa mnatutia wasiwasi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic