February 23, 2021


 KUREJEA kwa nyota wake sita ambao walikuwa nje ya kikosi cha Simba wakiongozwa na chaguo namba moja kwa Kocha Mkuu, Didier Gomes, kiungo, Rarry Bwalya, kumeongeza tabasamu kwa kocha huyo.

 

Bwalya na wachezaji wenzake watano ambao ni Jonas Mkude, Ibrahim Ame, Erasto Nyoni, Kennedy Juma na Ally Salim pamoja na meneja wa timu hiyo, Abas Ally, walibaki DR Congo kwa kile kilichoelezwa na mamlaka kuwa wana maambukizi ya Corona baada ya kumalizana na AS Vita.

 

Kwa sasa nyota hao tayari wamesharejea Bongo na walikuwa kwenye mazoezi rasmi na wenzao ikiwa ni maandalizi ya mechi yao ya kimataifa ya hatua ya makundi dhidi ya Al Ahly, Waarabu wa Misri, leo Februari 23 Uwanja wa Mkapa.


Kwenye orodha ya wachezaji hao ambao wameungana na timu hiyo, Bwalya amekuwa akipewa nafasi zaidi ambapo mbele ya TP Mazembe alitumia dakika 75, kwa Al Hilal na Dodoma Jiji alimaliza zote 90.

 

Dhidi ya Azam FC alitumia dakika 78 na AS Vita dakika 59.Jumla kwenye mechi sita ambazo Gomes ameongoza kikosi hicho, amekosekana kwenye mechi moja mbele ya Biashara United na ametumia dakika 392, hivyo kurejea kwake kumeongeza tabasamu kwa Gomes kuelekea mchezo wa leo.

 

Gomes amesema kuwa maandalizi yapo sawa na wanaamini kwamba itakuwa kazi kubwa kusaka ushindi ila wapo tayari kwa kuwa wamejipanga.


"Tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu ila tunatambua namna gani tunapaswa kufanya, kila kitu tunaamini kwamba kitakuwa sawa,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic