February 27, 2021

 


FT: Yanga 1-0 Ken Gold 

Mpira umekamilika Uwanja wa uhuru kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Ken Gold.

Ushindi huo unaifanya Yanga isonge mbele hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho.

Dakika 90 Niyonzima anafanya jaribio jepesi linaokolewa na kipa wa Ken Gold 
Dakika ya 88 Fiston anatoka anaingia anaingia Sarpong 
Dakika ya 80 Carinhos anaonyeshwa kadi nyekundu
Dakika ya 79 Carinhos anampiga ngumi mchezaji wa Ken Gold 
Dakika ya 78 Niyonzima anafanya jaribio linaokolewa na kipa wa Ken Gold 
Dakika ya 70 Yanga wanapata kona inapigwa na Carinhos 
Dakika ya 69 Shikalo anaokoa jaribio la Ken Gold 
Dakika ya 67 Carinhos anafanya jaribio linaokolewa na kipa wa Ken Gold 
Dakika ya 66 Carinhos anaingia anatoka Nchimbi 
Dakika ya 63  Ken Gold wanapoteza nafasi ya wazi ndani ya 18
Dakika ya 61 Fiston anakosa nafasi ndani ya 18
Dakika ya 59 Haruna anaingia anatoka Kaseke
Dakika ya 59 Yanga wanapata kona ya 10
Dakika ya 53 Fiston anakosa nafasi ya wazi
Dakika ya 50 Kaseke anaotea
Dakika ya 49 Nchimbi anamwaga majalo linaokolewa na kipa
Kipindi cha pili kimeanza 
UWANJA wa Uhuru

Kombe la Shirikisho,  hatua ya 32 bora


Yanga 0-1Ken Gold

Mapumziko,  Uwanja wa Uhuru

Dakika 42 Gooooal   Fiston

Dakika ya 40 Yanga wanapata Penalti 

Dakika ya 34 Kaseke anacheza faulo akiwa ndani ya 18 eneo la Ken Gold 

Dakika ya 32 Ken Gold wanapeleka mashambulizi kwa Shikhalo 

Dakika ya 31  Farid Mussa anafanya shambulizi ndani ya Ken Gold ila mpira unamzidi  spidi

Dakika ya 28 Kaseke anaotea 

Dakika ya 23 Fiston anafanya jaribio linaokolewa na kipa wa Ken Gold 

Dakika ya 16, Fei Toto anapaisha shuti lake akiwa nje ya 18

Dakika ya 12 Ken Gold wanakosa nafasi ya wazi ndani ya 18

Dakika ya 10 Nchimbi anakpsa nafasi ya wazi

Dakika 9 Farid Mussa anapiga faulo inaokolewa

Dakika ya 7 Nchimbi anapeleka mashambulizi Kengold anazuiwa

Dakika ya 4 Kengold wanapata faulo ya Kwanza  haileti matunda 

Dakika ya 3 Kengold wanapiga kona

13 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Mmmmmmh,jamani Yanga wanapata penalt, inapigwa na mchezaji wa Yanga kuelekezwa Ken Gold na anafifungia Yanga goli, halafu mwandishi unaandika Yanga 0 - 1 Ken Gold. Kweli?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahahahahahaha!!!!!!! Siamini kama ni matokeo ya shule za kata maana hata ambae ameishia la saba hawezi kutoa updates za kiutopolo namna hii

      Delete
  3. Mwandishi una haraka ya nini?

    ReplyDelete
  4. Mungu wangu tunakosea wapi?Timu haichezi kitimu kabisa. Tuna matatizo makubwa. Tuanze kusikiliza mawazo ya Sunday Manara ambaye leo akihojiwa amezungumza mengi yanayopaswa kufanyika kuhusu timu yetu.
    Haikubaliki kwa standard ya mpira tunaocheza.

    ReplyDelete
  5. Kwa kikosi kamili Yanga wapata goli la peneti dhidi ya timu ndogo isiyojulikana na huku nyota Kalihnyo anayetegemewa akipewa kadi nyekundu kwa kumpiga ngumi mchezaji wa timu pinzani kwa kosa lisilojulikana

    ReplyDelete
  6. Hapa ndipo tulipofika mabingwa wa jadi

    ReplyDelete
  7. Juma Mwambusi alikuwa hakubaliani na mbinu za Kaze na akawa anamshauri lakini ikaonekana anampinga mwisho wa jambo akaona isiwe tabu

    ReplyDelete
  8. Tutamkumbuka Juma Mwambusi.Tokea aondoke timu yetu imekuwa tia maji tia maji.

    ReplyDelete
  9. Wazee wa penalty kama kawaida yao hahahahaaaaaaaa

    ReplyDelete
  10. Shida wachezaji ni kama kumfundisha fisi kupanda mti.Miguu ya mbele mirefu kuliko ya nyuma.Itachukua muda,mrefu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic