BAADA YA KAMBI YA UTURUKI KUPIGWA MAJUNGU KISA PRISONS, SIMBA WAIBUKA NA TAMKO LAO
Kufuatia timu ya Simba kuibuka na ushindi kiduchu wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons juzi kwenye mchezo wa ufunguzi wa pazia la Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19, uongozi wa klabu hiyo umeibuka na tamko juu ya kambi ya Uturuki.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya kuibuka kwa kebehi na maneno juu ya kambi hiyo wakihoji imekuwa timu iweke kambi Uturuki halafu haipati matokeo ambayo hayaridhishi.
Kufuatia uwepo wa maneno hayo ikiwemo mitandaoni na kutoka upande wa pili ambao ni wa watani zao wa jadi Yanga, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara, ameibuka na kujibu kuwa hawakwenda nchini huko kujifunza mpira.
Manara ameeleza hayo baada ya kuona kejeli na na majungu vinazidi kushika kasi na kuamua kuja na jibu fupi pekee ili kuonesha kuwa anaona na kusikia kinachozungumzwa.
Ofisa huyo amesema lengo kubwa la kwenda Uturuki ilikuwa ni kuwandaa wachezaji kwa msimu mpya ujao na kuweza kuzoeana kutokana na baadhi kuwa wageni na wakiwa hawajazoeana.
Wakati Manara akieleza hayo, kikosi cha Simba hivi sasa kinajiandaa na mchezo mwingine wa ligi dhidi ya Mbeya City utakaopigwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
simba ijiangalie inapata kila kitu ila muunganiko wa wachezaji ni zero hivi yanga ndio ingekuwa kama simba ingekuwaje,tuache siasa na kebehi kwenye ukweli tuwe wakweli benchi la ufundi wana kitu cha kufanya kama ziada
ReplyDeleteusituletee uchura wako.....
DeleteAu ni kweli kule uturuki timu ilikuainacheza na madereva taxi
ReplyDeleteAu ni kweli kule uturuki timu ilikuainacheza na madereva taxi
ReplyDeleteTatizo la simba ni kuwa inapiga makelele sana kupitia kwa msemaji mwenye makelele sana..
ReplyDeleteMakelele ya simba na manara wake husababisha kukamiwa na kila timu..!!
Wanafanya vitu vya kawaida kama kusafiri kwa ndege, kula hotelini... lakini kwa kukosa busara wanahisi kuwa huko ndo kucheza soka..!!
kelele nyiiiingi tofauti na uwezo wa uwanjani.
DeleteHatari sana haya mambo! This is Simba bwana!
ReplyDeleteThis is Tanzania Bwana mahali ambapo kocha maarufu alipata kuitwa Sambusa mbovu badala ya Samsar... kisa timu ilikosa matokeo tarajiwa. Wenzetu wanafaulu kwa kupewa moyo "welldone ama well try" wanapoanguka ili wapate ujasiri zaidi sisi tunajua kuponda na ujuaji wa kulaumu kwa tusiyo na weledi nayo. Sitoshangaa Simba ikifanya vibaya katika ligi maana wanaotaka matokeo wanadhani Simba inacheza ligi na mashati.