February 9, 2021

 


KIUNGO mshambuliaji wa kikosi cha klabu ya Azam, Idd Selemani Nado ‘Idd Nado’ amefunguka kuwa namna rahisi ya kuwafunga Simba ni kufanya maamuzi ya haraka mbele ya safu yao ya ulinzi ambayo mara kwa mara hufanya makosa.

Nado alihusika katika mabao yote mawili waliyoyapata katika mchezo wa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba, katika mchezo wao wa kiporo uliopigwa siku ya Jumapili.

Akizungumzia mapungufu ya safu ya ulinzi ya Simba Nado alisema: “Simba ina wachezaji wengi bora ikiwemo mabeki wao hasa wa pembeni, Shomari Kapombe na Mohammed Hussein ‘Zimbwe’.

"Hivyo kama utahitaji kupata matokeo dhidi yao ni lazima uhakikishe unakuwa na maamuzi ya haraka dhidi yao pale wanapofanya makosa.

Sare hiyo ya Jumapili iliwafanya Azam kufikisha pointi 33 katika michezo yao 18 waliyocheza hivyo kusalia katika nafasi ya tatu ya msimamo.

 

9 COMMENTS:

  1. Huna lolote ww zaidi ya kuhtaji usajili! Na hatukusajili ht km ulitufunga!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndio wachezaji wa kibongo sijui mpaka sasa ana magoli mangapi siku akibahatisha ni makelele tupu

      Delete
  2. Hakuna lolote kelele tuu, sare tuu mnarap vile mngeshinda si mngekuwa nanyi mnasherehekea mitaani kama wa upande ule?

    ReplyDelete
  3. Basi wiki yote hii ni habari ya Simba kufunngwa na Naddo. Jifunzeni weledi jamani! Na Simba ingefungwa je? mngeandika mpaka mtoboe magazeti na hizi blog zenu

    ReplyDelete
  4. Je umewauliza Africa Lyon ukitaka wafinga Yanga mtu afanyeje.kili yako ni ndogo sana mwandishi..ushabiki wako hautakusaidia kitu.umeshinda unarudia kuhusu sare ya Simba mara kwa mara..na hapa kuna unafuu sababu siku moja kabla Yanga ilifungwa na Africa lyon pamoja na kuwa Africa Lyon walikuwa wampoteza kocha..tunategemea hii wiki yote utarudia habari hii kwa uandishi tofauti...maana akili yako imeishia hapo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ile ilikuwa mechi ya kirafiki sio ligi yanga kaapoteza nini nyie kiporo kimechacha naile kauli ya tunaongoza ligi kwa magoli haipo tenaa unaongozaje na mechi zako huja cheza mpira hauchezwi mdomoni

      Delete
    2. Heeeh heeh heeh.....kiporo kimechacha sasa mnaanza kutoa mapovu yaliyochacha pia.

      Delete
  5. Mipovu kama yote naona mnafulia kofuli zenu ha ha ha ha kama imekuuma chomoa ufute #team nyau

    ReplyDelete
  6. Hata kama ni mchezo wa kirafiki..Kama Simba ingekufungwa na Africa Lyon ndiyo ungekuwa wimbo wenu.. African Lyon iko daraja la ngapi? Si mmemchukua na kocha wao? Simba ina uwiano na Azam..wote wametoa sare na TP Mazembe..Isitoshe Simba ni ya Pili na Azam ni ya tatu katika ligi...Kiuhalisia hamuandiki kuhusu Yanga kufungwa wakati imefungwa na vibonde..tactic hambazo hazisaidii kabisa? jifunzeni basi..mwaka jana mlipoteza muda mwingi mkiandika yule muuaji wa Simba mara baada ya Morrison kuwafunga Simba..Je ilisaidia Yanga kupata ubingwa..Ongezeni basi akili zenu..acheni ujinga...haiwasaidii wala timu yenu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic