February 24, 2021


KLABU ya Namungo, ipo kwenye hatua za kujihakikishia kupata dola 275,000 (zaidi ya Sh milioni 635) kutoka Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

 

Hiyo itakamilika ikiwa itatinga hatua ya makundi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo hivi sasa inasubiri mechi ya marudiano dhidi ya CD Primeiro de Agosto itakayochezwa kesho Alhamisi kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar.


Katika mchezo wa kwanza, Namungo iliibuka na ushindi wa mabao 6-2, hivyo kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele na kutinga makundi ambapo inahitaji sare ya aina yoyote au ipoteze mechi kwa mabao yasiyozidi 4-0.

 

Fedha hizo zitatolewa na CAF kwa timu ambayo itashika nafasi ya mwisho kwenye kundi.Namungo ikitinga makundi, itakuwa Kundi D na timu za Nkana, Raja Club Athletic na Pyramids.


Hemed Morocco, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa mipango inakwenda sawa na wanaamini watapata ushindi kwenye mchezo huo.


"Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji ushindi, sisi tupo tayari na tunaamini kwamba tutapata matokeo chanya ndani ya uwanja,".

3 COMMENTS:

  1. NAMUNGO WASHAPITA TAYARI NA PESA ZISHAANDALIWA KWA AJILI YAO. SWALI LA KUJIULIZA WATAPITA KATIKA MIKONO YA HAWA WATU RJA CASABLANCA, PYRAMIDS? MAANA HAWA SIO KMC HIZI NI TIMU ZA GHARAMA ZAIDI YA NKANA RANGERS..........WAKATI UTATUPA MAJIBU

    ReplyDelete
  2. Kwahatua waliofikia wana hitaji kupongezwa kuna mwaka Azam fc iliishia mwanzoni kabsa,,,makundi walisikia radioni tu,,,mi nawapa big up yakutosha

    ReplyDelete
  3. Wame jitahidi japo leo wame poteza mchezo 👏👏👏👏

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic