April 24, 2019


Uongozi wa timu ya KMC FC kutoka Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam umesema kuwa umewasoma vizuri wapinzani wao Simba katika mchezo waliocheza jana dhidi ya Alliance Schools wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa Radio One, Ofisa Habari wa timu hiyo, Anuary Mbinde, amesema kuwa waliutazama mchezo huo kupitia runinga na waliona mbinu walizozitumia Simba na kuahidi kuzifanyia kazi kuelekea mechi ijayo.

"Tuliutazama mchezo wao kupitia runinga, hatukwenda Uwanjani.

"Tumeshapata mbinu zao, tumejipanga vizuri kuelekea mchezo huo."

Simba na KMC zinakutana kesho palepale kwenye Uwanja wa CCM Kirumba majira ya saa 10 kamili za jioni huku mechi hiyo ikiwa ni ya aina yake.

Katika msimamo wa ligi inaonesha Simba wako nafasi ya tatu wakiwa na alama 63 huku wakicheza jumla ya michezi 25.

Wakati huo KMC nao wako nafasi ya 7 wakiwa wamecheza jumla ya michezo 32 huku wakijikusanyia jumla ya pointi 42.

Mechi hiyo inakuwa ya aina yake kutokana na Simba kuhitaji zaidi matokeo kwani ipo kwenye harakati za kutetea ubingwa wake huku Alliance ikiwa haina cha kupoteza hivi sasa hata kama ikifungwa.


5 COMMENTS:

  1. Alliance tena haina cha kupoteza? Waandishi nyie umakini haupo kabisa!

    ReplyDelete
  2. Lakini si uliona wachezaji wa Simba jana nusu yake ni wachezaji wa akiba? na hao,waliobaki ndio mtaopambana nao. Tumbe Salama

    ReplyDelete
  3. Hata Simba Haina Cha Kupoteza Kama Pesa Caf Wanatupa Ambayo Halingani Na Hiyo TPL

    ReplyDelete
  4. Simba ndo yakusema mme isoma bax mtaisoma mkicheza nayo na mtaisoma namba ambayo Ni magori

    ReplyDelete
  5. Alliance tena. Copy paste ni nshidaaaaa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic