February 9, 2021


BEKI wa zamani wa Klabu ya Simba, Boniface Pawasa amesema kuwa ili Simba iweze kutusua kimataifa ni lazima iwe na kiungo mkabaji makini ambaye atakuwa anatuliza mipira pamoja na hatari ndani ya uwanja.

Simba kwa sasa ina viungo wakabaji wawili ambao ni chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu, Didier Gomes, Mzamiru Yassin na Thadeo Lwanga huku Jonas Mkude na Said Ndemla wakiwa bado hawajapata nafasi kwenye kikosi chake.

Leo kikosi kinatarajia kukwea pipa kuelekea Congo majira ya saa 10:00 jioni ambapo kina mchezo wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi dhidi ya AS Vita unaotarajiwa kuchezwa Februari 12.

Akizungumza na Saleh Jembe, Pawasa ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya Ufukweni, amesema kuwa kila kitu kinawezekana ikiwa watakuwa na kiungo mkabaji makini.

"Kwenye mechi za kimataifa ni muhimu kuwa na kiungo mkabaji mwenye nguvu na uwezo wa kukaa na mpira muda mwingi jambo litakalopunguza mashambulizi kwa upande wao.

"Kwa namna ambavyo nimeona kikosi cha Simba kikiwa na Lwanga bado kuna kitu kinahitajika kwa upande wa kiungo mkabaji kwa kuwa ulimwengu wa mpira umebadilika.

"Nimemuona Lwanga naona bado anajitahidi ila hajawa kwenye ule ubora wake ambao ninaujua. Ninawajua wachezaji wanaotoka Uganda ni watu wa nguvu sana hivyo ni suala la kusubiri na kuona namna gani inaweza kuwa," amesema.

1 COMMENTS:

  1. Simba ilipaswa kulivalia njuga swala la mkongo kiungo mkabaji Doxa Gakanji.Sioni sababu ya kumkosa wakati Congo ilitolewa Chan tarehe 30/01 na walikuwa na masaa 24 kabla ya dirisha la usajili wa CAF kufungwa 31/01

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic