VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wakiwa na pointi zao 44
baada ya kucheza jumla ya mechi 18 wana kazi ya kufunga mwezi Februari kwa
kusaka pointi tisa kwenye mechi zao tatu za moto.
Ina mechi tatu za kusaka pointi tisa ambazo ni dakika 270 za kibabe ndani ya uwanja ndani ya Februari.
Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze itaanza kazi ugenini
mbele ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine, Februari 13. Kwenye mchezo wa kwanza
uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Yanga ilishinda bao 1-0.
Ikimaliza kazi Mbeya itarejea Dar ambapo itakutana na Kagera
Sugar, Uwanja wa Mkapa, Februari 17 ikiwa na kumbukumbu ya kushinda bao 1-0
mchezo wa kwanza Uwanja wa Kaitaba.
Itafunga kazi ndani ya Februari kwa kumenyana Mtibwa Sugar,
Februari 20, Uwanja wa Mkapa na ilipowafuata pale Jamhuri, Morogoro ilishinda
bao 1-0.
Kaze ameliambia Spoti Xtra kuwa wana kazi ngumu ya kufanya
kusaka pointi tatu kwani hayo ni malengo ambayo wamejiwekea.
0 COMMENTS:
Post a Comment