February 10, 2021


 WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa, Simba wameweka wazi kwamba wanaamini watafanya vizuri kimataifa kwa kuanza na mchezo wao dhidi ya AS Vita.

Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa wanatambua wana kazi kubwa ya kufanya kimataifa hilo lipo wazi na mipango yao inakwenda sawa.

Februari 12 itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya AS Vita ambayo wapo nayo kwenye kundi A utakaochezwa Uwanja wa Stade des Martyrs.

Simba ina kumbukumbu ya kufungwa mabao 5-0 ilipokutana na AS Vita zama zile za Patrick Aussem kwenye hatua ya makundi jambo ambalo wameweka wazi kwamba halitajirudia.

Leo Februari 10 kikosi kinatarajia kuwasili Congo kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa kimataifa ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

“Tunajua kwamba tuna kazi ya kufanya kimataifa hilo lipo wazi kikubwa ambacho tunaamini ni kwamba tutafanya vizuri.Uwepo wa wachezaji wenye uzoefu pamoja na ari waliyonayo wachezaji ni silaha kwetu kufanya vizuri, hivyo mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Ndani ya kundi A ambapo wapo Simba na wapinzani wao AS Vita pia ipo timu ya Al Ahly pamoja na Al-Merrikh.

1 COMMENTS:

  1. Kwa hiyo ulitaka wasijipe matumaini? Basi wajipe matumaini hao walio fungwa juzi vyura ambao hukuandika habari yao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic