February 10, 2021



DAVID Moyes, Kocha Mkuu wa West Ham United amesema kuwa wakati wakichapwa bao 1-0 dhidi ya Manchester United mchezo wa Kombe la FA walistahili kufika Kwenye hatua ya kupigiana penalti.

Moyes amesisitiza kuwa majeruhi wa kikosi cha kwanza ndani ya West Ham United yamewapa nguvu Manchester United kupata ushindi kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Old Trafford. 

Bao la Scott McTominay katika muda wa nyongeza baada ya dakika 90 za awali kukamilika bila mshindi kupatikana liliwaondoa jumlajumla West Ham United kwenye mbio za kuweza kutinga hatua ya robo fainali na lilipachikwa dakika ya 97.

Kocha huyo amesema kwenye muda wa nyongeza uliotolewa walitakiwa kufanya mambo mawili kutumia nafasi ambazo wamezipata ama kulinda wasifungwe ila kwa kuwa wapinzani wao walikuwa imara ikawa ngumu kwao kushinda jambo lililowaondoa mapema.

"Ninawapongeza wachezaji wangu wamepambana na kuonyesha ushindani, haikuwa rahisi ila majeruhi kwenye kikosi changu yamechangia nishindwe kupata ushindi.

"Kwenye muda wa nyongeza tulikuwa na nafasi mbili ila tulishindwa kuzigeuza kuwa bao na mwisho wa siku wapinzani wetu wamepata nafasi wakaitumia ingekuwa tumekazana tangu mwanzo tulikuwa na nafasi ya kufika kwenye hatua ya penalti," .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic