February 9, 2021

 


KWENYE mchezo wa Klabu Bingwa hatua ya nusu fainali, uliochezwa usiku wa kuamkia leo Klabu ya Al Ahly ya Misri ambayo ipo kundi moja na Klabu ya Simba ya Tanzania imepoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Bayern Munich. 

Mabao ya Bayern Munich ambayo imetinga hatua ya fainali yalifungwa na mshambuliaji wao bora Robert Lewandowski dakika ya 17 na 85 na kuipeleka timu yake hatua ya fainali.

Wakiwa Uwanja wa Al Rayyan wapinzani hao wa Simba waliopo pamoja kwenye kundi A, waliweza kupiga jumla ya mashuti 5 huku Bayern Munich wakipiga jumla ya mashuti 24 ambapo ni mashuti 7 yalilenga lango huku kwa Al Ahly yalilenga lango mashuti mawili.

Upande wa umiliki wa mpira, Al Ahly ilikuwa na asilimia 31 huku Munich ikiwa na asilimia 69 hivyo Simba ina kazi ya kufanya itakapokutana na wapinzani hawa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, Februari 23, Uwanja wa Mkapa.

Bayern Munich itacheza fainali ya Klabu Bingwa Duniani dhidi ya Club Tigres UANL ya Mexico, Februari 11,2020 huku Al Ahly ya Misri ikitarajiwa kucheza mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu dhidi RSB Berkane, Februari 17.

6 COMMENTS:

  1. Duuh!!inaanza fainali halafu inakuja mshindi wa tatu

    ReplyDelete
  2. February 16, Al Ahly atakuwa uwanja wa nyumbani kwao akicheza mechi ya kwanza ya CAF Champion League!

    ReplyDelete
  3. Manake mikia wanahairishiwa Ligi kwa sababu zipi?

    ReplyDelete
  4. Jipimeni tena na African Sport ya Tanga na wala msikubali kujipima na timu kama zile ambazo waheshimiwa Simba waljipima kwa hofu ya kufungwa

    ReplyDelete
  5. Mpira haupimwi kwa kuangalia matokeo ya wengine, kama ndio hivyo mbona Azam alipigwa na Yanga Simba aka drop au Ruvushooting alipigwa na Yanga lkn aka mka mpakata Simba?

    ReplyDelete
  6. Simba hata acheze na jiwe mm nashabikia jiwe t

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic