February 9, 2021


 UONGOZI wa Klabu ya Azam FC umesema kuwa haujawahi kufungwa kihalali na wapinzani wao Simba ndani ya dakika 90 kwenye mechi walizokutana nao uwanjani.


Februari 7, Azam FC walilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Simba na kugawana pointi mojamoja Uwanja wa Mkapa.

Zakaria Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kwenye mechi hizo tano ambazo walifungwa na Simba ni mechi moja walifungwa kihalali.

 "Katika mechi tano walizotufunga, naweza kusema ni moja tu walitufunga kihalali na ni ile ya FA ambayo kiujumla hatukuwa vizuri, nyingine ile ya mapinduzi tunajua penalti hazina mwenyewe.


"Ila Mechi tatu zote zilizosalia walibebwa na waamuzi, Kuna bao walitufunga mpira ulikuwa umetoka nje, ile nyingine Idd Chilunda alisawazisha mwamuzi akakataa, nyingine walifunga bao la offside wao wakakubali," .

Simba imefikisha jumla ya pointi 39 kibindoni baada ya kucheza jumla ya mechi 17 huku Azam FC ikiwa na pointi 33 ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo.

11 COMMENTS:

  1. Huo sasa ni ubishi wa kitoto. Matokep yakishaandikwa ndio hayo, kuleta longo longo leo mi upuuzi wa kishamba tuu. Ungekata rufaa kwa hayo unayozusha leo.

    ReplyDelete
  2. Basi sawa, azam kamfunga simba mara zote, furahi wewe.

    ReplyDelete
  3. Huyu Zakazaka iko siku mdomo wake utamponza....

    ReplyDelete
  4. Siku zote usitoe jasho lako kubishana na mjinga vinginevyo ukiendelea kubishana na mjinga basi jamii haitaelewa ni nani mjinga na mpumbafu kati yenu.Mwacheni huyo jinga Zakazaka kwani anatetea kibarua chake.

    ReplyDelete
  5. Simba na Yanga hubebwa sana na waamuzi, hilo halina ubishi!Manokata mna maslahi ya kiushbiki tu.

    ReplyDelete
  6. KWA SABABU HAJUI MPIRA, NA HAPO WALIPO WANAJUA HAWAWEZI KUTWAA UBINGWA. WAMEMHUJUMU CIOBA, STEWART HALL, ITAKUWA KUACHA KUSEMA UKWELI JUU YA HALI ZAO? MAKOCHA WOTE WA KIZUNGU AZAM FC PALE WANAHUJUMIWA. ARSTICA CIOBA MSIMU HUU ALISHAJIPANGA BUT KUNA WAPUUZI MLE NDANI YA TIMU WAKAFANYA YAO, TIMU INA SHINDA MECHI 7 MFULULIZO MNASEMA KOCHA MBOVU INAINGIA AKILINI?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Alitimuliwa baada ya kufungwa kihalali na Yanga

      Delete
  7. Huo no ukweli Hiyo wote tuliona marefa wanajiripuaga hasa mechi za wenye TFF

    ReplyDelete
  8. Tatizo linalowapa kiburi ni hiyo sare ya kubahatisha

    ReplyDelete
  9. Angesema wamefungwa kihali mechi zote mapovu ya singewatoka kusema vile tu mnaanza kumtukana sio vizuri ule ni mtizamo wake yeye ndivyo anavyoamini yeye

    ReplyDelete
  10. Sijajua elimu yako ya journalism, lkn nadhani ni duni sana! Una hata diploma wewe? Yafaa urudi tena shule na uzee wako huohuo! Msemaji wa timu unasema vitu vya ajabu kama hivi!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic