KUELEKEA kwenye mchezo wa leo Machi 16, Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi kati ya Simba dhidi ya Al Merrikh, Kocha Mkuu wa wapinzani wa Simba, Lee Clark amesema kuwa vijana wake wapo tayari kupata ushindi leo.
Maneno hayo ni ujumbe mzito kwa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ambaye naye anahitaji pointi tatu pia.
Mchezo wa leo kwa Simba utakuwa na ushindani mkubwa kwa sababu Al Merrikh inahitaji kufufua matumaini ya kutinga hatua ya robo fainali huku Simba nao wakihitaji nafasi hiyo.
Kundi A kwa sasa halina mwenyewe kwa kuwa kinara Simba ana pointi 7, AS Vita na Al Ahly wana pointi nne nao wanacheza leo pia, huku Al Merrikh akiwa na pointi moja kwa namna yoyote akishinda matumaini yanarejea ya kufuzu.
Clark amesema: "Maandalizi ni mazuri na tupo tayari vijana wanahitaji ushindi hakuna lingine, kwa namna yoyote ile tutapambana ili kupata ushindi".
NA MTASHINDA LEO BILA UBISHI
ReplyDeleteWATASHINDA NA NJAA,KUNA WAKATI WA KULIA NA WAKATI WAKUOMBOLEZA,NINGEKUSHAURI UNGEENDA KULE VICHOCHORONI UKAENDELEE KUNYWA GONGO NA WANZUKI,NA KWA TAARIFA YAKO HATA HAO AS VITA WANAKUFA KWAO LEO NA SIO SIMBA,MTANZANIA GANI WEWE USIE NA AKILI HATA UKUBWA WA CHEMBE YA VUMBI,MAFANIKIO YA SIMBA YATAKUBEBA HATA WEWE LAKIN UNASHNDWA KUJIONGEZA,SUBIRI MUDA UTAONGEA BABA.
DeleteAiwezekan m2 kuxhda kwa mkapa
ReplyDeleteAiwezekan m2 kuxhda kwa mkapa
ReplyDeleteAiwezekan m2 kuxhda kwa mkapa
ReplyDeleteLet them know that a battalion of hungry mighty eleven lions eager waiting for them
ReplyDeleteHalafu hili suala la kuzuia mashabiki wasiingie kbs mimi haliniingii akilini, Kama suala ni corona kwa nn wasiweke utaratibu wa kuingiza mashabiki kidogo Kisha wakae mbalimbali. Hizi zitakuwa figisu za Ahly maana baada ya kupigwa na Mnyama wakaanza kulalamika juu ya mashabiki. Pia Kuna habar kuwa leo Vita wamepanga kuingiza mashabiki 2000 ingawa Ahly wanagomea
ReplyDelete