UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa msimu huu hautatoka
mikono mitupu kama ilivyokuwa msimu uliopita wa 2019/20.
Ujumbe huo unaingia moja kwa moja kwa mabingwa watetezi wa
Kombe la Shirikisho pamoja na Ligi Kuu Bara, Simba ambao nao wameweka wazi
kwamba wanahitaji kutetea mataji yao yanayopigiwa hesabu pia na vinara wa ligi,
Yanga.
“Tuna kikosi kizuri chenye wachezaji makini ambao wanajituma
ndani ya uwanja, kwa namna ambavyo ushindani unakwenda na namna tunavyopata
matokeo mazuri hatutatoka mikono mitupu.
“Malengo ni kuona tunatwaa mataji mawili ama moja kati ya
haya makubwa lile la ligi pamoja na Kombe la Shirikisho, tunahitaji kurejea
kimataifa na hilo linawezekana mashabiki watupe sapoti,” alisema.
Kinara wa utupiaji ni Prince Dube mwenye mabao saba ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na George Lwandamina.
WAPAMBANE NA HALI ZAO TU, WAICHEZE KUIFUNGA SIMBA WACHEZE KUTAFUTA MAKOMBE. WANATOA SARE NA SIMBA WANAENDA KUFUNGWA NA COASTAL UNION WAKATI SIMBA ANAIFUNGA AS VITA. HIVI HAMUONI KUWA MNATOFAUTIANA MALENGO?
ReplyDeletena wewe uliemfunga VITA vipi ulifungwa na prison
DeleteSiku zote vitani huwa anaangaliwa Alie kuzidi nguvu. Huwezi ukamfikiria mgambo badala ya kumfikiria komando
DeleteMashabiki watupe sapoti timu inacheza madudu
ReplyDeleteNdivyo wanavyojifariji na madudu yao.
ReplyDeletePambana.
ReplyDelete