BAKARI Mwanyeto anatajwa kuwekwa kando kwa muda ndani ya kikosi cha Yanga ili kumpisha nyota mpya Dikson Job kwenye upande wa safu ya ulinzi.
Mwamnyeto amekuwa akifanya kazi kwa ushirikiano na mshikaji wake Lamine Moro kwenye kulinda ngome ya Yanga ila wamekuwa wakifanya makosa ambayo yanaigharimu timu hiyo.
Kwenye mechi dhidi ya Kagera Sugar, Uwanja wa Mkapa wakati wakiokota jumla ya mabao matatu unafanya iwe rekodi yao ya kwanza msimu huu kuokota mabao mengi nyavuni kwenye mchezo mmoja.
Pia walikwama kuweka umakini wakati walipokutana na Coastal Union, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga Machi 4.
Baada ya dakika 90, ubao wa pale Mkwakwani ulisoma Coastal Union 2-1 Yanga jambo lililofanya timu hiyo inayonolewa na Cedric Kaze kupoteza mchezo wake wa kwanza kwenye ligi.
Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa tayari Job ambaye ni ingizo jipya kutoka ndani ya Mtibwa Sugar ameanza kufanya mazoezi mepesi na atakabidhiwa majukumu ya Mwamnyeto.
"Kijana Job yupo tayari kuanza kucheza mechi za ushindani kwa kuwa majeruhi aliyokuwa anasumbuliwa nayo yamepona na ameanza mazoezi mepesi.
"Ana jukumu la kubeba mikoba ya Mwamnyeto kwa muda ili kuweza kumpa nafasi ya kupumzika kwa kuwa hajawa sawa kisaikolojia baada ya kupata matatizo ya kifamilia, " ilieleza taarifa hiyo.
Cedric Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa kupoteza kwao kunatokana na makosa ambayo wanayafanya uwanjani hivyo watayafanyia kazi.
Huu sio uandishi mzuri. Unaposema kuwekwa kando haileti picha nzuri kwa mwamnyeto, itamvunja moyo kijana, bora useme job anakuja kumpa changamoto, akiweza kumpoka namba hilo halina ubishi ndio mpira. Sio kuwekana kando kienyeji au kihasira hasira
ReplyDeleteAliyeandika haya si kocha bali ni mfazamo mbaya wa mwandishi uchwara. Awekwe kando kisa kipi? You are not serious with your work
DeleteMwamnyeto hawezi kukaa benchi hata akija kwetu Simba bado hawezi kukaa benchi kufungwa ni kawaida,ukisema akae benchi kisa kafungwa basi hata washambuliaji wote wa yanga wakae benchi mbona hawafungi.mwandishi umekuwa masikini wa habari.
ReplyDeleteHAPANA SIO KOSA LA MANDISHI ILA NI MAKOSA YA KIUFUNDI TU, MWANDISHI ANA RIPOTI KILE AMBACHO KIANAENDELEA. INGEBIDI KAZE ABADILI SAFU YOTE YA ULINZI TU
DeleteHawa waandishi humu sijui wamewaokota wapi yani hovyo kbs hawajui hata jinsi ya kuandika taarifa. Kila siku wanakosolewa lkn hata hawajifunzi.
ReplyDeleteKwan kaze ndo kampa taalifa kuwa nondo atasugua baenchi?au nimaono take tu KWA vile kaona jobu kapona
ReplyDeleteHuyu Mwamnyetu alijikosesha yeye mwenyewe kujiunga na timu sugu ya matatizo na timu ambayo imekuwa daima wachezaji wakishitaki kwa kutolipwa haki zao. Mwamnyetu ni kati ya wslinzi bora kabisa nchini lakini sasa hivi imefika hadi kutengwa jambo litalopelekea kushuka kiwango na kuonekana hafai. Kama hakuzinduka mapema ka Kakolanya basi mustakbali wake kimpira utaingia gizani
ReplyDelete